Mazungumzo ….. Ni njia ya kufikia masuluhisho
Bw. Hassan Ghazaly-Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana
Ni sura mojawapo ya sura za kukaribiana kiutamaduni, ambapo mapokezi yetu ya mwaka wa kimisri wa kisasa kwa namba (6264) yatokea sambamba na sherehe ya Ethiopia ya (Inkotach) kwa Mwaka Mpya wa Ethiopia Nambar (2015), kama inavyojulikana kuwa Ethiopia hutumia kalenda tofauti na nyingi za ulimwengu kote, na kalenda ya Ethiopia asili yake inatokana na kalenda ya Al-Shamsi ya kimisri basi inaongeza siku ya ziada kwa miaka yote bila tofauti, hiyo ndiyo inayozingatiwa maelewano mengine kati ya raia wetu wema.
Picha hii inanikusanya mimi pamoja na rafiki yangu mpendwa wa Ethiopia “Tezgerida Zwedo,” Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Ethiopia, ambaye nina urafiki naye kwa zaidi ya miaka 8.
Kutoka kumbukumbu ya picha, wakati wa mkutano wetu pembezoni mwa mojawapo ya makongamano ya mashauriano ya viongozi wa vijana waafrika ambapo nilikuwa mwakilishi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kama mtaalamu wa bara katika masuala ya harakati na mashirika ya vijana.
Labda sisi, kama wanadiplomasia wa vijana, tulikubaliana kwamba hakuna njia ya kufikia suluhisho kwa matatizo yetu ya nchi mbili na masuala yetu ya kiafrika isipokuwa tu tukutane juu ya meza moja ya majadiliano, tukiamini kwamba mazungumzo ni mbinu muhimu zaidi ambao utuwezeshe kufikia mitazamo karibu, kuunga mkono na kuimarisha mahusiano kati ya raia.
Ninaamini kwa nguvu na nia yetu kama vijana kuunda historia nzuri na kwa uwezo wetu wa kushughulikia shida yoyote na kufikia suluhisho kwake, na kuacha kwetu kwa kiburi, upekwe na upendeleo bila ufahamu wa kina kwa matokeo yanayowezekana kusababishwa na mambo mnamo siku zijazo, na vizazi vyetu vijavyo vitakavyoyakumba .
Daima Misri na watu wake huamini kwa dhana ya amani inayotegemea kweli bila kutia chumvi au kuacha kabisa.
“Misri ni kijiji changu…Afrika ni nchi ya nyumbani mwangu”