Vijana Na Michezo

CAF yamtuza Rais El Sisi Tuzo ya Kifahari kwa Mafanikio Bora kwa Mwaka 2024

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), linaloongozwa na Patrice Motsepe, limeamua kutoa tuzo ya juu kabisa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), tuzo ya kifahari kwa mafanikio bora kwa mwaka 2024, kwa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, Hii ni kwa kutambua juhudi bora na mchango mkubwa katika maendeleo na ukuaji wa soka nchini Misri na bara la Afrika kupitia maendeleo ya miundombinu na vifaa tofauti vya mpira wa miguu vimevyojengwa nchini Misri, na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo na ukuaji wa soka nchini Misri na Bara la Afrika.

Waziri wa Vijana na Michezo, Dkt. Ashraf Sobhy  anatarajiwa kukabidhiwa tuzo hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wakati wa sherehe za kila mwaka za tuzo za CAF za mwaka 2024 zinazorushwa moja kwa moja kwa nchi zaidi ya 100 Duniani, leo Jumatatu Desemba 16, 2024 nchini Morocco.

Back to top button