Makala za maoni

JENGA HOJA USIPIGE KELELE: MASLAHI YA TAIFA

Muongozo Rasmi wa Utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje kutoka kwa Rais.
Tafsiri imefanywa na Abbas Mwalimu.
Mwalimu Nyerere anasema;
“Ndani ya mfumo wa amani na ushirikiano wa kimataifa tunahitaji na tunatamani, hivyo, tunapaswa kukubali kuwa Serikali ya Tanzania ndiyo serikali pekee ambayo jambo kuu la msingi inayoshughulishwa nalo ni maslahi ya watu wa Tanzania, kama ilivyo kwa Serikali ya Marekani ni serikali pekee ambayo jambo kuu inayoshughulishwa nayo ni maslahi ya watu wa Marekani, serikali ya Urusi kwa warusi, serikali ya China kwa wachina, na kadhalika.”
Nchi nyingine-nyingi kati yao-zinaweza kuwa na malengo na maslahi ambayo Tanzania pia inayo.
Takribani nchi zote hizo zitakuwa na malengo mengine ambayo hayafanani na yetu, hata kama sisi si maadui kwao.
Lakini si Tanzania au nchi nyingine yoyote duniani inaweza kukwepa uhalisia huu wa kila nchi kutazama maslahi ya watu wake kwanza katika dunia hii.
Hivyo, ni katika muktadha huo wa mfumo wa muunganiko wa kiteknolojia lakini tukiwa tumegawanyika kisiasa kwamba sisi katika Tanzania tunapaswa kufahamu malengo yetu na kuamua ni kwa namna gani nzuri tunaweza kuyafikia malengo hayo.”
Abbas Mwalimu
Abbas Mwalimu
Back to top button