Baba Tawadros II, Baba wa Alexandria, Patriaki wa Jimbo la Mtakatifu Marko, kwenye makao makuu ya Baba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Marko huko Abbasiya, Leo alikutana na Mtukufu Imamu, Dkt Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al-Azhar Al-Shareif, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na ujumbe kutoka kwa Usheikh wa Al-Azhar, na pamoja nao Mheshimiwa Dkt. Ali Gomaa, Mufti Mkuu wa zamani wa Misri.
Imamu na msafara wake walitoa pongezi zao za dhati kwa Utakatifu wake(Mtukufu Wake) katika hafla ya Krismasi Njema.