Uncategorized

Ushirikiano wa Kilimo na kubadilishana uzoefu kati ya Misri na Tanzania Waziri wa Kilimo na kugeuza Ardhi ” Al Said Al_Qusair ” aliwapokea Waziri wa Mifugo wa Uvuvi

Ushirikiano wa Kilimo na kubadilishana uzoefu kati ya Misri na Tanzania
Waziri wa Kilimo na kugeuza Ardhi ” Al Said Al_Qusair ” aliwapokea Waziri wa Mifugo wa Uvuvi

” Mashimba Nadaky” na ujumbe wake, Na alijadili naye njia za Ushirikiano kati ya nchi ndugu hizo mbili kwa mahudhurio ya Mhandisi ” Mostafa Alsayad” Naibu wa Waziri wa Kilimo wa kuku, uvuvi na mifugo, na mwenyekiti na viongozi wa kampuni ya Uvuvi wa kitaifa na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Kilimo.

Katika mkutano huo, Al_Qusair alimkaribisha waziri wa Tanzania na alisema kuwa Misri ina uzoefu mkubwa na majaribio yenye mafanikio katika uwanja wa uvuvi na mifugo, ambapo inashika nafasi ya kwanza katika ufugaji wa samaki barani Afrika, ya sita Duniani,na ya tatu katika uzalishaji wa Bolty Duniani kote na tuna miradi mikubwa katika Uvuvi na vifaranga vya maji.

na inawezekana kufaidika kutoka uzoefu wa Misri katika uwanja wa ufungaji wa samaki katika bahari na majisafi, iwe kwa mfumo wa vizimba vya bahari vilivyofunga au kwa mfumo wa Bonde, pamoja na kuwepo kwa nafasi ya ushirikiano katika uwanja wa meli na boti za Uvuvi, vilevile magonjwa ya samaki, ambapo Misri ikishughulikia kwa muda mrefu katika uwanja huo wa uzoefu wa kiufundi.

 

Na Al_Qusair aliongeza kuwa inawezekana kushirikiana na Tanzania katika uwanja wa kuzalisha Dawa na chanjo pia makundi ya mifugo na pia mafunzo na kujenga uwezo, mauzo ya nje na kuanzisha mashamba ya pamoja, haswa Misri ina shamba la uzalishaji wa mimea huko Zanzibar.

Na Al_Qusair aliashiria umuhimu wa kutekeleza mkataba wa maelewano uliosainiwa baina ya nchi mbili mwaka wa 2018 katika uwanja wa mimea, uzalishaji wa mifugo na uvuvi, uboreshaji wa maumbile na nyanja zingine tofauti za kilimo.

Waziri wa Kilimo alisisitiza pia ushirikiano katika uwanja wa utafiti uliotumika, ambapo Misri ina vyuo na vituo vya utafiti vya kipekee pamoja na taasisi ya sayansi ya bahari na Uvuvi na Kitivo maalum cha uvuvi, na pia alisisitiza uwezekano wa ushirikiano katika uwanja wa kutengeneza chakula cha mifugo.

Kwa upande wake, Waziri wa uzalishaji Mifugo na Uvuvi wa Tanzania ” Mashimba Nadaky” ameeleza furaha yake ya kutembelea Misri na mapokezi hayo mema, akiashiria nia ya nchi yake ya kusukuma hatua za ushirikiano na Misri haswa katika uwanja wa mifugo,Dawa na chanjo za mifugo, ambapo Tanzania inashika nafasi ya pili barani Afrika katika idadi ya mifugo na ina takriban mifugo milioni 34.

Back to top button