Habari

Wanafunzi 50 kutoka nchi za Bonde la Nile ni wahitimu wa uwanja wa kuboresha Sekta ya Umeme

0:00

Katika uthibitisho wa maoni na maelekezo ya Rais Abd El Fatah El-Sisi ya kuimarisha mahusiano ya ushirikiano na nchi za kiafrika, Dokta. Mohamed Shaker, Waziri wa Umeme na Nishati ya kudumu, na baadhi ya viongozi wa sekta hiyo, walihudhuria Alhamisi asubuhi tarehe 24/2 sherehe ya kuhitimu wanafunzi 50 kutoka nchi za Bonde la Nile katika programu tano za mafunzo chini ya kichwa “Mipango ya miradi na tathmini ya Athari kwa mazingira”, “Vihamisho kwa njia za upitishaji Umeme wa msongo wa juu”, “Uendeshaji na matengenezo ya mitandao ya usambazaji”, “Mifumo ya Kinga. ”, na “Uongozi wa miradi”.

Dokta. Shaker ameeleza kuwa programu hizo za mafunzo zilijumuisha wanafunzi”50″ kutoka nchi za Bonde la Nile nchini Sudan, Djibouti, Burundi, Somalia na Uganda.

Aliongeza kuwa programu hizo zinakuja ndani ya kozi kadhaa za mafunzo zinazotekelezwa ndani ya mfumo wa mradi wa ushirikiano na nchi za kiafrika, unaochukuliwa na sekta hiyo na unatekelezwa kujenga uwezo wa kibinadamu katika nchi za Bonde la Nile katika nyanja za Umeme nchini Misri. , iwe kupitia programu za mafunzo au kwa kutuma wataalam wa Misri kwa nchi hizo katika nyanja mbalimbali za nishati.

Katika sherehe hiyo Dokta.Shaker alitoa hotuba ambapo aliwakaribisha ndugu hao wa Afrika akiwakilisha serikali ya Misri na kwa niaba yake binafsi ndani ya mfumo wa miradi ya Ushirikiano na nchi za Afrika ili kuimarisha mahusiano kati ya nchi za Bara zima.

Na DoKta.Shaker alisisitiza umuhimu wa vyanzo vya binadamu, ambayo ni sehemu muhimu ya Shirika lolote, ambayo inatufanya wakati wote tufanye kazi ya kuwekeza katika uwezo wa binadamu na kuandaa programu za kujenga na kuboresha uwezo huo ili kuendana na mabadiliko ya haraka na yanayoendelea katika sekta ya Umeme na kwa ajili ya kudumisha Ufanisi wa uwezo wa binadamu uliopo.

pia amesisitiza kuwa programu za kuunda uwezo na kubadilishana uzoefu ni jambo la muhimu sana kwa ajili ya kuunga mkono na kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi na kufikia Ushirikiano wa kweli ili kuhakikisha manufaa ya pamoja na malengo yanayotarajiwa.

Na katika suala hilo, Misri ilichukua hatua ya kuanzisha mfumo wa kazi ya Taasisi ili kuhakikisha malengo yake kwa kupitia Ufadhili wa Misri kwa Ushirikiano wa kiufundi na Afrika.

Pia alisisitiza kuwa Misri inathamini asili ya kiafrika na inafahamu vyema changamoto za pamoja zinazolikabili bara hilo, akieleza uangalifu wa kudumu wa Misri ya kufanya kazi kwa pamoja na nchi za bara la Afrika ili kuhakikisha mipango yenye matarajio na haki ya kisheria ya nchi zote za bara hilo kufurahia Amani, Utulivu, Ustawi na Maendeleo endelevu.

Na DoKta. Shaker alisisitiza utayari wa sekta ya Umeme wa Misri kutoa msaada wa kiufundi na kutoa utaalamu wake kwa ndugu katika nchi za Afrika, akielezea Shukrani zake kwa Ushirikiano wa kipekee na wenye manufaa kati ya Misri na nchi kadhaa za Afrika katika kuunda uwezo, ambapo sekta ya Umeme na ya nishati ya kudumu ya Misri ilifanikiwa kuandaa na kutekeleza programu za mafunzo kwa wanafunzi 8,417 wa Kiafrika, akiashiria kwa Sekta ya Umeme ya Misri ina zaidi ya vituo 20 vya mafunzo, viwili kati yao vimepata ithibati kutoka kwa Jumuiya ya Huduma za Nishati Afrika (APUA) Aidha,Oktoba 2018 , mkataba wa makubaliano ulitiwa saini na COMESA katika uwanja wa mafunzo na kuunda uwezo.

Kwa upande wao, wanafunzi hao walitoa Shukrani kwa nafasi na juhudi kubwa zinazofanywa na sekta ya Umeme na nishati ya Misri katika uandaaji na mpango wa kozi za mafunzo ili kupata manufaa makubwa kutoka kwao, huku wakisisitiza kuwa watafanya kazi ya kutoa uzoefu walioupata kutoka Misri hadi nchi yao, wakisisitiza manufaa walioyapata kutoka programu hizo, ambapo kozi hizo za mafunzo zilijumuisha ziara kadhaa zenye lengo la kufuata maendeleo ya kazi kwa maeneo ya miradi ya Umeme na makampuni ya Misri yanayofanya kazi katika uwanja wa kutengeneza kazi za Umeme.pia maeneo kadhaa ya Utalii nchini Misri.

Ikumbukwe kuwa kozi za mafunzo zinazotolewa na Wizara ya Umeme na Nishati ya kudumu kwa wanafunzi 8,417 kutoka Afrika zilijumuisha kozi kadhaa zinaonekana kama usaidizi wa masomo, ambapo Wizara ilibeba thamani zote za mafunzo, makazi na tiketi za ndege kwa kupitia mradi wa Ushirikiano na nchi za kiafrika,ambapo kiasi cha programu za mafunzo zimefika 159, na warsha 4 za kutoa mafunzo kwa wanafunzwa 2,437 (kutoka nchi 26 za Afrika na mashirika mawili) katika nyanja za uzalishaji, uhamisho na usambazaji wa Umeme, nishati ya kudumu na Ufanisi wa nishati.

Pia Wizara imetuma takriban wataalamu 39 wa Misri kutoka sekta hiyo kwa nchi kadhaa za Afrika (Sudan, Rwanda, Tanzania, Burundi, Somalia, Eritrea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) ili kuhamisha utaalamu kwa nchi hizo, kutoa msaada wa kiufundi na kusaidia nchi hizo kuandaa mipango yao ya kitaifa, haswa katika uwanja wa nishati ya kudumu.

Back to top button