Uncategorized

FUNGUA DIMBA TAMISEMI YAWANYOOSHA UCHUKUZI 31 -16

Asila Twaha, Iringa

Timu ya wanawake netiboli TAMISEMI imefungua ndimba kwa kuwanyoosha wapinzani wake timu ya uchukuzi goli 31-16 katika Mashindano ya Michezo ya Shirikisho ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea Mkoani Iringa.

Mechi iliyochezwa leo  katika viwanja vya Chuo cha RUAHA majira ya saa tisa jioni timu ya TAMISEMI ilicheza na wapinzani wake timu ya uchukuzi  mpaka muda wa mapunziko TAMISEMI ilikuwa inaongoza goli 17-7.

Kocha wa Timu ya TAMISEMI Maimuna Kitete amesema timu yake ipo vizuri na ndio mechi ya kwanza  ambapo wachezaji wameonesha uwezo mkubwa ijapokuwa ndio ilikuwa mechi ya kwanza  hata kwa upande wa  timu pinzani amesema ilikuwa ipo vizuri lakini timu ya TAMISEMI ilicheza kwa kujituma  na kwa kiwango kikubwa zaidi na mpaka mechi inaisha walishinda goli 31-16.

Amesema  timu  ipo  hatua ya makundi ambapo timu ya TAMISEMI ipo kundi E na imepangwa kucheza mechi nne na kwa mechi waliocheza ya kwanza wamepata pointi 2 ambapo hawajapoteza pointi hata moja.

Naye Kapteni wa Timu ya TAMISEMI netiboli Dafrosa Luwhago amesema, wanaendelea na ushirikiano sababu bila ya kuwa na umoja ushindi hauwezi kupatikana sababu kila timu imejipanga kuchukua ushindi.

“Ninawashukuru sana viongozi wangu wa Wizara kwa kutuwezesha kushiriki mashindano haya lakini na wachezaji wenzangu kwa kuendelea kujituma katika michezo na mazoezi” Dafrosa.

Back to top button