Uncategorized

MHE. MCHENGERWA AKUTANA NA VIONGOZI WA TAPSEA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na viongozi wa chama cha Waandishi Waendesha Ofisi zaman wakijulikana kama Makatibu Mahutasi (TAPSEA) kwenye Ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo Jijini Dar ea salaam leo tarehe 20.12.2023.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mchengerwa amesema umekua wakati mzuri kukutana na viongozi hao kwani Kada ya Waandishi Waendesha Ofisi ni muhimu sana kwa viongozi kuweza kufanikisha kazi zao kwani wamekua wasaidizi wa karibu wa viongozi katika Utumishi wa Umma.

Amesema hoja zote zilizowasilishwa na viongozi hao zitafanyiwa kazi na amemuelekeza Katibu Mkuu kuhakikisha kuwa Waandishi Waendesha Ofisi kutoka kwenye Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wanashiriki kikamilifu katika vikao vya TAPSEA vinavyofanyika kila mwaka nchini.

Amesema anaunga mkono suala la kutoa mafunzo kwa wataalam hao kwa kuwa yatawaongezea uwezo wa kufanya kazi kwa weledi na kwa wale wanaotoka kwenye Tawala za Mikoa wataelekezwa kushiriki kwenye mafunzo hayo.

Aidha ameainisha kuwa changamoto ya ada ya ushiriki iliyowasilishwa kuwa wakipewa maafisa hao kulipia vikao wengi huwa hawafikishi hivyo wale wote waliochini yake amemuelekeza Katibu Mkuu kulipa michango hiyo moja kwa moja kwenye chama hicho.

Naye Mwenyekiti wa TAPSEA Taifa Bi. Zuhura Songambele Maganga amesema wamekuja kujitambulisha na kuelekezea mikakati yao kwa mwaka unaokuja ili wanachama wa TAPSEA waweze kushiriki kwa wingi katika kikao kitakachokuja.

Back to top button