Mwalimu Nyerere anasema:
“Malengo haya tunayoyaendea hayabadiliki na si mambo ambayo tunaweza kukubali kuingia kwenye maelewano fulani ili kuyaachia.
Kitu kitakachobadilika kila baada ya muda fulani, na ambacho kinaweza kuwekwa kwenye majadiliano na mazungumzo, ni mbinu tunazotumia katika kuyaendea malengo hayo.
Ni kama vile timu ya mpira wa miguu inavyofanyia kazi mbinu zake katika kufikia malengo yake (ambayo ni kushinda mechi bila shaka) mazingira katika uwanja, uimara na udhaifu wa timu zote mbili, na kadhalika, hivyo basi Tanzania ni lazima ifanyie kazi mbinu zake kwa kuzingatia malengo yake na mazingira halisi yanayojitokeza.
Ni lazima tuelewe malengo yetu na yanamaanisha nini: ni lazima tuielewe dunia tunayoishi ilivyo na hapo ni lazima tutafute njia bora za kukuza malengo yetu kwa kuzingatia mazingira yaliyopo.”
Itaendelea sehemu ya kumi na moja .