Wizara ya Mambo ya Nje Pamoja na mabalozi wa kikundi cha kiafrika watafutia Usafirishaji kuelekea Mji mkuu wa utawala
Katika muktadha wa maandalizi ili kusafirisha kwa mji mkuu mpya wa utawala, Balozi Yasser Reda, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje kwa masuala ya kifedha, na usimamizi, pia masuala ya ofisi kuu na mji mkuu mpya wa utawala aliendelea
Mtiririko wa mikutano inayofanikiwa mara kwa mara pamoja na Balozi za kigeni na Mashirika ya kimataifa yaliyoidhinishwa huko nchini Misri, ambapo aliwakaribisha kikundi cha mabalozi wa nchi za Kiafrika kinachojumuisha mabalozi wa Algeria Angola, Ghana, Guinea, Mauritius, Morocco, Msumbiji, Rwanda, Tanzania, Tunisia na Zambia.
Balozi Yasser Reda alionesha maandalizi ya serikali ya kimisri ili kusafirisha mji mkuu wa utawala, akidokeza
Kasi ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Mambo ya Nje katika maandalizi ya kufikia pale kikamilifu,
Akitoa wito kwa mabalozi wa nchi za Kiafrika kwa ziara ya vituo vya mji mkuu wa utawala Miongoni mwao ni wilaya ya serikali, majengo ya Wizara kuu, Bunge, Wizara ya Mambo ya Nje, Mtaa wa kidiplomasia, msikiti wa Misri na Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Kristo,yanayozingatiwa miongoni mwa maeneo makubwa ya ibada Duniani. Pamoja na Mji wa sanaa unaojumuisha Maktaba ya mji mkuu
Makumbusho ya Miji mikuu ya Misri na Nyumba mpya ya Opera.
Balozi alieleza huduma na Vifaa vilivyotolewa na mji mkuu mpya wa utawala kwa upande wa mawasiliano rahisi na Wizara katika wilaya ya serikali, Mtaa wa kidiplomasia, miundombinu ya kisasa, huduma mbalimbali, vituo vya elimu na afya na vituo vya biashara, utamaduni na burudani.
Balozi Yasser Reda alisisitiza kufurahia Misri kwa utambulisho wa kiafrika, na nia ya Misri juu ya kuimarisha mahusiano ya urafiki na ushirikiano katika nyanja zote , pamoja na nchi za kirafiki katika Barani Afrika. Akiashiria maandalizi kamili ya Wizara ya mambo ya Nje ili Kujibu maswali yote ya ndugu zetu katika balozi za Afrika na kutoa msaada kwa aina zake zote ili kuwezesha uhamisho wa balozi za nchi hizo dada kwa mji mkuu mpya wa utawala, inayoonyesha mwanzo mpya wa Misri ambao unathibitisha mafanikio yaliyopatikana katika miaka iliyopita na kuanzisha siku za Usoni za Misri ya baadaye.