Misri yasisitiza Uungaji mkono wake kwa juhudi za Uenezaji wa Utulivu nchini Somalia

Dokta Mohamed Gad Balozi wa Jamhuri ya kiarabu ya Misri nchini Ethiopia na mwakilishi wake wa kudumu kwa Umoja wa Afrika alishiriki katika kikao cha Baraza la Amani na Usalama wa Afrika, kilichofanyika jana kwa ajili ya kujadili maandalizi baada ya ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya kuhifadhi Amani nchini Somalia (AMISOM) inayokuja katika mfumo wa kufuatilia maendeleo kwa upande wa Mashauriano kati ya Umoja wa Afrika na Serikali ya Somalia katika Suala hilo.
Balozi wa Misri – kulingana na Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje- katika kauli yake amekaribisha maendeleo ya Mashauriano na pendekezo la muundo ya ujumbe wa mpito kwa Umoja wa Afrika nchini Somalia akiashiria kikao kilichofanyika katika Kituo cha Kairo cha Kimataifa kwa ajili ya kusuluhisha migogoro na kuhifadhi na ujenzi wa Amani Mjini Cairo mnamo Januari iliyopita na kushiriki kwake katika kukaribisha maoni na kutumia Pendekezo hilo vizuri.
Na pia Dokta Mohamed Gad alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa ujumbe uliopendekezwa kama pendekezo la ujumla katika kukabiliana na changamoto nchini Somalia na katika upanuzi wa vipengele vyake polisi na raia na kuunga mkono uwezo wa Taasisi za Usalama za Somalia na pia kushiriki kwake katika juhudi za ujenzi unaohakikisha uendelevu wa Utulivu, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa ratiba ya wakati na viashirio maalum kwa kuhamisha jukumu la Usalama kikamilifu kuelekea Taasisi ya nchi ya Somalia, kama utekelezaji wa mpango wa Mabadiliko wa Somalia.
Na mwishoni mwa kikao, kulikuwa na kipaumbele cha kuutambulisha ujumbe mpya wa mabadiliko kwa wajibu wa kuunga mkono wa uwezo wa Somalia na kuthibitisha kuwa kuhifadhi Umoja na Uhuru wa Somalia na Ufuatiliaji wa Baraza kwa maendeleo husika na pendekezo la ujumbe mpya na matokeo ya Mashauriano pamoja na Baraza la Usalama la kimataifa kuhusu Suala hilo.