Habari Tofauti
DKT. MSONDE AINGIA DARASANI KUFUNDISHA, KUPIMA UTEKELEZAJI WA KPI
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde akifundisha somo la hesabu wanafunzi wa darasa la Saba katika shule ya Msingi Ulaya iliyopo katika halmashauri ya wilaya Igunga Mkoani Tabora.
Leo tarehe 28 Agosti 2023, Dkt. Msonde anaendelea na ziara ya kukagua hali ya utoaji wa elimu mashuleni na kukagua utekeleza wa vigezo vya kuboresha elimu nchini (KPI).
Aidha, Dkt. Msonde alitaka kujihakikishia utayari wa wanafunzi hao wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtiani wa kuhutimu elimu ya msingi mwezi Septemba 2023.