Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Adolf Ndunguru amesema Serikali imeendelea kusimamia na kuhakikisha fedha zinatengwa na kutolewa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo kwa wastani wa kitaifa kwa mwaka wa fedha 2022/23 tumefikia asilimia 86.69 ya utekelezaji wa bajeti ya lishe ukilinganisha na asilimia 22 ya mwaka wa fedha 2017/18 wakati kunasaini Mkataba wa lishe nchini.
Ameeleza hayo wakati akitoa mrejesho wa utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kipindi cha Julai, 2022 hadi Juni, 2023, uliosainiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa niaba ya Mheshimiwa Rais tangu Desemba, 2017 kwenye mkutano wa Tathmini ya saba ya utekelezaji wa mkataba wa lishe unaofanyika katika ukumbi wa Jiji la Dodoma, Mtumba jijini Dodoma
Amezitaja Halmashauri tano ambazo haikuweza kuchangia fedha hizo kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mkalama, Uyui na Lushoto nakuziagiza kuhakikisha kufanyia mapitio ya bajenti ya mwezi Disemba na kuingiza fedha inayotakiwa kukidhi matakwa ya Serikali ya kutenga kiasi cha shilingi 1000 kwa watoto walio chini ya miaka mitano.
Aidha, amesema kumekuwa na ongezeko la bajeti ya shughuli za Lishe katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutoka shilingi bilioni 13.5 kwa mwaka wa fedha 2022/23 hadi bilioni 14.8 kwa mwaka wa fedha 2023/24.