Habari Tofauti

Mawaziri wa Elimu ya Juu na Afya washiriki katika mkutano wa maandalizi ya uzinduzi wa toleo la pili la Mkutano wa Tiba wa Afrika kwa Mwaka wa 2023

Ali Mahmoud

Dkt. Ayman Ashour, Waziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Kisayansi, Dkt. Khaled Abdel Ghaffar, Waziri wa Afya na Makazi, walishiriki katika mkutano wa maandalizi ya uzinduzi wa toleo la pili la maonesho na mkutano wa Afya ya Afrika “Africa Health ExCon 2023”, ikiwa na kauli mbiu “Lango Lako kuelekea Uvumbuzi na Biashara”, ulioandaliwa na Mamlaka ya Misri ya Ununuzi wenye Umoja, usambazaji wa matibabu na usimamizi wa teknolojia ya tiba, pamoja na uangalizi wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, mnamo kipindi cha kuanzia 7 hadi 10 Juni ijayo huko Kairo.

Dkt. Ayman Ashour alisifu mafanikio ya toleo la kwanza la mkutano huo mnamo mwaka uliopita kwa sababu ya msaada usio na kifani wa uongozi wa kisiasa, akiashiria jukumu muhimu la maendeleo la mkutano huo katika kushughulikia na changamoto na shida zinazokabili Bara la Afrika katika uwanja wa huduma za afya, akisisitiza kuwa mkutano huo katika toleo lake la pili utatumika kama jukwaa la mazungumzo kati ya vyombo vya utafiti katika nchi za kiafrika kubadilishana uzoefu kati yao, kuratibu na kampuni za kimataifa kusaidia katika kukuza masuluhisho kwa shida za afya Barani Afrika, pamoja na kufanya kazi kuchunguza nafasi zinazopatikana za uwekezaji na biashara katika sekta ya afya Barani Afrika.

Dkt. Ayman Ashour alisisitiza umuhimu wa jukumu la kuunga mkono na ushiriki wa Vyuo Vikuu vyote na hospitali zao, Baraza Kuu la Hospitali za Chuo Kikuu, vituo, taasisi na mashirika ya utafiti ya Misri na ya kiafrika katika shughuli za toleo la pili la mkutano huo kwa kuzingatia mihimili yake na ajenda yake ya kisayansi, ili kufikia ushirikiano zaidi na kubadilishana uzoefu kati yao, na kujadili masuala muhimu zaidi katika kiwango cha vifaa vya matibabu na huduma za afya, akielezea kuwa hii ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za kufikia mfumo bora wa sayansi za Afya katika Bara la Afrika, ambao kwa upande wake unachangia mchakato wa maendeleo na mwamko unaopatikana katika nchi mbalimbali za Bara.

Waziri wa Elimu ya Juu alisisitiza umuhimu wa kuandaa kwa mkutano huo kwa njia inayofaa hadhi ya Misri katika ngazi za kimataifa na za kiafrika, na kuendana na Maoni ya Misri 2030, akiashiria umuhimu wa mkutano huo katika kukuza maendeleo endelevu ya watu wa Afrika, ambayo moja ya misingi yao kuu ni kutoa maisha salama yenye afya kwa raia, haswa kwa kuzingatia kile ambacho maeneo mengi ya bara hilo yanakabiliwa na kuenea kwa magonjwa, na inahitaji juhudi za pamoja za wana wake kufikia uboreshaji zaidi wa huduma ya afya iliyotolewa, akitakia mkutano huo mwaka huu mafanikio makubwa na kufikia malengo yake yanayotarajiwa.

Dkt. Khaled Abdul Ghaffar, Waziri wa Afya na Wakazi, alithibitisha kuwa Mheshimiwa Rais, Abdel Fattah El-Sisi, hulipa kipaumbele kikubwa na msaada halisi kwa Maonesho na Mkutano wa Matibabu ya Afrika na “Africa Health EXCON 2023”, ambapo inawakilisha nguvu ya kisayansi na uwekezaji katika ngazi zote za afya, zikiongozwa na nyanja za viwanda vya dawa na matengenezo ya matibabu, akiashiria kuwa ni nafasi ya kubadilishana maono na kuunganisha uwezo wa afya katika nchi za bara la Afrika pamoja.

Dkt. Khalid Abdul Ghaffar alimshukuru Meja Jenerali Bahaa El-Din Zeidan, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Ununuzi wenye Umoja, na vyombo na sekta zote zinazohusika na kuandaa mkutano na maonesho katika toleo lake la pili, akithamini juhudi zao na nia ya kuungana pamoja kuandaa na kutekeleza maonesho katika toleo lake la pili mwaka huu, kulingana na mpango na maoni yaliyopangwa ya mkakati na yanayofaa hadhi ya Misri ndani na kimataifa.

Waziri wa Afya alisisitiza kuwa mkutano huo unakuja katika mfumo wa kuimarisha maoni ya Umoja katika ngazi ya sekta ya matibabu na ya afya katika bara la Afrika, pamoja na kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu na ujuzi katika uwanja wa huduma za afya, akibainisha kuwa ni lango la kuvutia uwekezaji wa afya na kujenga uwezo wa ushindani kati ya makampuni makubwa ya kimataifa katika uwanja wa afya Barani Afrika, akisisitiza kuwa nchi ya Misri inataka kubadilishana uzoefu na fursa za uwekezaji na nchi zote ndugu za Afrika; kujenga mfumo wa afya unaoweza kukabiliana na migogoro katika nchi nyingi za bara zinazokabiliwa na kuenea kwa magonjwa ya kipuku na magonjwa sugu.

Dkt. Khalid Abdul Ghaffar aliongeza kuwa mkutano wa maandalizi unashuhudia ushirikiano mkubwa, kubadilishana majadiliano na maoni; kuweka viwango na mipango madhubuti inayolenga kukamilisha hatua za mafanikio yaliyopatikana na Misri, kupitia uzinduzi wa upainia na nguvu kwa toleo la pili la mkutano 2023, akiashiria kuwa maonesho na mkutano wa matibabu wa kiafrika utashuhudia wakati wa kikao chake kijacho kujadili kile kilichopatikana ardhini tangu kumalizika kwa toleo la kwanza, ambalo lilifanikiwa kuunda mahitaji ya Afrika ya kurekebisha na kuboresha mfumo wa huduma za afya.

Waziri wa Afya na Makazi aliashiria kuwa wizara hiyo inafanya kazi Pamoja na Mamlaka ya Ununuzi wenye Umoja kwa lengo la kusaidia nchi za kiafrika kudumisha huduma za afya na kuletea bara utaalam unaohitajika kujenga kubadilika katika mifumo ya huduma za afya, haswa kwa kuzingatia kushuka kwa uchumi mwingi kama matokeo ya janga la Corona.

Kwa upande wake, Meja Jenerali Bahaa El-Din Zeidan, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Misri ya Ununuzi wenye Umoja, Ugavi wa Tiba na Teknolojia ya Tiba, aliashiria kuwa mafanikio ya mkutano huo katika toleo lake la kwanza yanatokana na ushirikiano na mshikamano kati ya mamlaka husika, akieleza kuwa mkutano huo mwaka huu unalenga wageni na washiriki 60,000 kutoka kwa wawakilishi wa sekta za afya katika nchi 100 duniani, pamoja na uwepo wa washiriki 3,000 kutoka kwa mawaziri, wakuu wa makampuni, wawakilishi wa serikali, watoa maamuzi, na waanzilishi wa viwanda vya matibabu barani Afrika na Mashariki ya Kati; kujadili na kutafuta changamoto zinazozikabili nchi za Afrika katika sekta ya afya, kugundua fursa mbalimbali za uwekezaji, pamoja na kutafuta njia za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za bara hilo kutoa na kushirikisha viwanda vya dawa, vituo vya matengenezo ya matibabu, pamoja na waoneshaji 500 na washiriki 300 kutoka kwa watoa maamuzi.

Dkt. Awad Taj El-Din, Mshauri wa Rais wa Jamhuri kwa Masuala ya Afya na Kinga, aliashiria umuhimu wa mkutano huo kwani ni jukwaa la utangulizi kwa wajumbe wanaoshiriki kutoka nchi mbalimbali duniani, huku vituo vikubwa na vya juu vya afya vya Misri, pamoja na makampuni makubwa yanayofanya kazi katika nyanja za dawa na vifaa vya tiba nchini Misri, na pia ni fursa ya kuanzisha ushirikiano mpya na wenye matokeo kati ya nchi mbalimbali Duniani katika uwanja wa huduma za afya, kwa njia inayoonekana katika ustawi kwenye mifumo yote ya afya ya Afrika, akisisitiza haja ya kuzingatia utalii wa matibabu, na kufanya kazi kwa ujanibishaji halisi wa kutengeneza Dawa, vyombo na vifaa tiba, kama moja ya changamoto kubwa inayoikabili Afrika, pamoja na kuvutia kampuni za kimataifa kuanzisha vituo vya matengenezo ya vifaa vya tiba.

Kwa upande wake, Dkt. Adel Adawi, Waziri wa zamani sana wa Afya na Wakazi, Mkuu wa Chama cha Madaktari wa Misri, alisisitiza kuwa udhamini wa uongozi wa kisiasa wa mkutano huo unawakilisha msaada mkubwa kwa mafanikio yake, akiashiria kuwa kazi inafanyika kuandaa mpango wa kisayansi wa mkutano huo unaozingatia changamoto zilizopo katika uwanja wa afya, vyombo na vifaa tiba, akiashiria umuhimu wa kunufaika na uzoefu wa nchi zilizoendelea Duniani katika uwanja wa kuendeleza huduma za afya, ambapo ndivyo mkutano huu unavyoshughulikia, akieleza kuwa Maonesho na Mkutano wa Matibabu wa Afrika utatumika kama soko la kuvutia kwa dawa, huduma za utunzaji na vifaa vya tiba vya kila aina.

Wakati Dkt. Tamer Essam, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Dawa nchini Misri, akieleza kuwa mkutano wa maandalizi unatoa ujumbe wazi wa umuhimu wa Mkutano wa Tiba wa Afrika, na kwamba unaendana na hadhi ya Misri katika ngazi ya sekta ya afya, akieleza kuwa mkutano huu umekuwa kama njia endelevu ya mawasiliano na kila kitu kipya katika uwanja wa afya, na kwamba mkutano huu wa Afrika unachangia kuendeleza maono ya pamoja na kuratibu majadiliano mazuri ya bara ambayo yanachangia kubadilishana uzoefu na habari, kusaidia ubunifu na utafiti wa kisayansi katika sekta ya afya na dawa, na kuchochea biashara ya ndani ya Afrika kwa bidhaa kuu katika viwanda vya dawa na vifaa vya tiba.

Dkt. Ahmed Al-Sobky, Mkuu wa Mamlaka Kuu ya Huduma za Afya, aliishukuru Mamlaka ya Ununuzi wenye Umoja kwa juhudi zake za kuandaa toleo la kwanza la mkutano huo, na kuandaa toleo lake la pili, akiashiria kuwa mkutano huo utatumika kama lango la Misri kufikia uongozi katika sekta ya afya katika ngazi ya Bara la Afrika, na jukwaa la kuonesha mafanikio ya taifa la Misri katika uwanja wa viwanda vya vifaa vya afya, pamoja na kutoa mwanga juu ya uwezo unaofurahiwa na bara la Afrika, haswa Misri katika uwanja wa utalii wa matibabu.

Dkt. Al-Sobki amesisitiza kuwa Mkutano huo katika toleo lake la pili litazingatia mada mbalimbali muhimu ikiwemo usimamizi wa mifumo ya afya, uchumi katika huduma za afya, utawala katika huduma za kliniki, pamoja na kuzingatia mada bunifu, akibainisha kuwa mkutano huo utafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendeleza ushirikiano, uwekezaji na biashara kati ya nchi za Bara la Afrika.

Kando ya mkutano huo, Mamlaka ya Ununuzi wenye Umoja ilisaini itifaki ya ushirikiano na kundi la Hospitali za Saudi Ujerumani, ambapo Meja Jenerali Bahaa El-Din Zeidan alitia saini kwa upande wa Mamlaka, na kwa upande wa «Saudi Ujerumani» Dkt. Muhammad Hablas, Mkurugenzi Mtendaji wa «Saudi Ujerumani», chini ya kichwa «Africa Health EXCON Award», ili kamati iundwe katika ngazi ya Afrika kutathmini miradi ya matibabu itakayowasilishwa katika mkutano huo, na kuwapa mradi bora wa afya.

Inatajwa kuwa mkutano huo katika toleo lake la kwanza Mwaka uliopita ulishuhudia mafanikio yasiyo ya kawaida, kwa kushirikisha zaidi ya wageni 43,000 kutoka nchi 75, pamoja na kuandaa zaidi ya matukio 350 ya kisayansi, mahudhurio ya washirika 15 wa kimataifa, waoneshaji 368, wadhamini 64, ushiriki wa zaidi ya wazungumzaji na wataalamu wa kimataifa 800 katika uwanja wa matibabu, na watoa maamuzi 2,000 kutoka kwa wawakilishi wa huduma za afya katika nchi za Afrika.

Back to top button