
Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje Ijumaa Februari 24, ilikaribisha idhini ya Bunge la Libya la kurekebisha tangazo la 13 la katiba, kama hatua muhimu katika ngazi ya kutimiza mifumo muhimu ya kufanyika Uchaguzi wa Urais na wa Bunge wa Libya wakati huo huo haraka iwezekanavyo, chini ya usimamizi wa mamlaka ya utendaji isiyoegemea upande wowote inayoshikilia maslahi kuu ya nchi ndugu ya Libya.
Misri ilisisitiza matarajio yake kwa Mabaraza mawili ya Wawakilishi na Serikali ya Libya kukamilisha juhudi zao katika ngazi ya kuandaa sheria za uchaguzi, na kupitishwa na Bunge.
Taarifa hiyo ilisisitiza msaada kamili wa Misri kwa njia ya suluhisho la Libya- Libya, ikisifu juhudi za Bunge, mamlaka pekee ya kutunga sheria iliyochaguliwa nchini Libya, na Baraza kuu la Serikali, na kukataliwa kwake kwa maagizo yoyote ya nje kwa ndugu wa Libya au kupuuza jukumu la taasisi za Libya kulingana na marejeleo ya makubaliano ya Skhirat, ikitoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mzozo wa Libya kufuata misingi hii na viamua ambavyo havina mbadala.
Misri pia ilisisitiza hitaji la kusimamisha uingiliaji wa kigeni nchini Libya, kuondoka kwa vikosi vyote vya kigeni, wapiganaji wa kigeni na mamluki kutoka kwake, na uungaji mkono wake kwa misheni ya Kamati Husika ya Pamoja ya Jeshi 5+5 kuhakikishia uhuru na utulivu wa Libya.