Mawaziri wa Umwagiliaji wa Misri na Sudan Kusini wazindua kituo cha maji ya kunywa ya chini ya ardhi katika Mlima wa Lemon huko Mji mkuu Juba
Ali Mahmoud
** Waziri wa Umwagiliaji wa Sudan Kusini atoa shukrani zake kwa Misri kwa msaada wake unaotolewa kwa Sudan Kusini, haswa katika uwanja wa kutoa maji ya kunywa, inayochangia utulivu wa wananchi na kupunguza migogoro.
Dkt. Sewilam:
– Nafurahi kwa kuwepo kwangu kati ya watu wa Sudan Kusini na kusherehekea nao kwa uzinduzi wa maji kutoka kituo cha maji ya kunywa kilichotolewa na watu wa Misri kwa watu ndugu wa Sudan Kusini.
– Kituo hicho chabeba mema na maendeleo kwa wananchi wa eneo hilo na kinahudumia karibu watu 2,000.
– Misri imetekeleza vituo 20 vya maji ya kunywa ya chini ya ardhi katika maeneo ya mbali na kuviwasha kwa nishati ya jua kutoa maji ya kunywa kwa karibu watu 100,000.
– Utekelezaji wa miradi ya kuvuna maji ya mvua, kupunguza hatari za mafuriko na kusafisha mapito ya maji ya magugu.
– kipindi kijacho kitashuhudia miradi zaidi ya maendeleo katika majimbo mbalimbali ya Sudan Kusini.
– Kutoa pongezi kwa kumbukumbu ya Bw. Manawa Peter, Waziri marehemu wa Umwagiliaji wa Sudan Kusini, na mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwenye sherehe kubwa ya kitaifa .. Mheshimiwa Prof. Hani Sewilam, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, na Mheshimiwa Pal Mai Deng, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Jamhuri ya Sudan Kusini, walizindua kituo cha maji ya kunywa ya chini ya ardhi katika eneo la makazi kwenye Mlima Limon (moja ya vitongoji vilivyopo mashariki ya Mji mkuu, Juba) huku kukiwa na makaribisho na furaha kubwa kutoka kwa wananchi katika kitongoji, kwa mahudhurio ya Bw. Balozi Moataz Mustafa Abdel Qader, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa Sudan Kusini na kundi la viongozi na maafisa kutoka nchi hizo mbili.
Katika hotuba yake kwenye sherehe .. Dkt. Sewilam alielezea furaha yake kwa kuwepo kati ya watu wa nchi ndugu ya Sudan Kusini na kusherehekea nao kwa uzinduzi wa maji kutoka kituo cha maji ya kunywa kilichotolewa na watu wa Misri kwa watu ndugu wa Sudan Kusini, na ambacho hubeba mema na maendeleo kwa wananchi katika eneo ambacho chahudumia karibu watu 2,000 akielezea furaha yake binafsi kuona athari za kituo hicho kwa wananchi.
Mheshimiwa Waziri alisema kuwa Misri imekamilisha utekelezaji wa vituo 20 vya maji ya kunywa ya chini ya ardhi katika maeneo ya na kuviendesha kwa nishati ya jua kufikia uendelevu wa uendeshaji wake na kutoa maji ya kunywa kwa karibu watu 100,000 pamoja na utekelezaji wa miradi mingi ya kuvuna maji ya mvua, kupunguza hatari za mafuriko na kazi za kusafisha mapito ya maji kutoka katika magugu kuwezesha urambazaji wa mito na kuchochea biashara, ndani ya mfumo wa msaada wa kudumu wa Misri kwa Jamhuri ya Sudan Kusini kutekeleza miradi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Dkt. Sewilam alisisitiza kuwa mahusiano ya Misri na Sudan Kusini ni ya kina na yenye muda mrefu katika ngazi zote na kwa miaka mingi wakati ambapo miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa ambayo inawanufaisha moja kwa moja wananchi wa nchi ya Sudan Kusini, akisisitiza kuwa kipindi kijacho kitashuhudia miradi zaidi ya maendeleo katika majimbo mbalimbali ya Sudan Kusini.
Dkt. Sewilam alisifu kumbukumbu ya Bw. Manawa Peter, Waziri marehemu wa Rasilimali za Maji na umwagiliaji wa Sudan Kusini, na jukumu lake kubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa rasilimali za maji na umwagiliaji.
Katika hotuba yake, Bw. Pal Mai Deng alielezea furaha yake kwa ziara ya Dkt. Sewilam, na akitoa shukrani zake kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa msaada wake uliotolewa kwa Jamhuri ya Sudan Kusini, haswa katika uwanja wa kutoa maji safi ya kunywa kwa wananchi, inayochangia utulivu wa wananchi na kupunguza migogoro.