Utamduni
Mpango wa Afro-Media wajadili Vitabu viwili vya NJIANI & Karatasi Na Kalamu
0:00
Jumatano, Februari mosi Mpango wa vyombo vya habari Afro-Media unajadili Kitabu cha <<Karatasi Na Kalamu>> kilichoandikwa na Mfasiri na Mtangazaji Menna Yasser Desouki, Mtafiti mhusika wa Lugha za kiafrika.
Karatasi Na Kalamu.
Ni mkusanyiko wa hadithi fupi na mambo mengi ambayo tunayaishi kila siku, bila ya kuangalia umuhimu wake.
Na kutokana na umuhimu huo, Kitabu cha “Karatasi Na Kalamu ” chajadili baadhi ya maadili kuu maishani mwetu kama hadithi fupi, na mwishoni mwa kila hadithi tuwe na maadili, ambayo yanatuwezesha kuanza mara nyingine na kufikia mafanikio maishani mwetu.
Kuwepo kwa Karatasi Na Kalamu ni kitu muhimu sana maishani; tuweze kuhifadhi yote yenye thamani kubwa.
Hayo yote ni pamoja na kujadili Kitabu chake kingine “NJIANI” kinachojadili mambo kadhaa ya maendeleo ya binadamu. Duniani kuna mambo, kuna yanayojulikana na yasiyojulikana, naye binadamu huyo ni miongoni mwa mambo yale, binadamu ni msingi mkubwa sana maishani.
Ndani ya kitabu hicho pamoja tutazungumzia Maendeleo na Ustawi ambazo ni nguzo thabiti maishani, lakini hivyo itakua tofauti sana, ndio maana hatutazungumzia maendeleo ya uchumi au kile kinachohusiana na pesa au hata mahusiano ya nchi, hatutafanya hivyo kamwe, nao wanaodai kuwa maendeleo ni ya mambo hayo tu, napenda kuwaambia kuwa hivyo sivyo kabisa.
Sisi tuna la muhimu zaidi kuliko hayo yote,nayo ni binadamu binafsi, awamu za maendeleo yake, kujiboresha, jinsi anavyowaza, tajriba zake binafsi,vikwazo vinavyokwamisha kufikia malengo yake, jinsi ya kushinda changamoto hizo, yaani tutazungumzia mengine mengi ndani ya hiki kitabu <<NJIANI>>.