Utamduni

“Kwa Jina la Misri pamoja twasoma, twafikiri, twajenga”.. Kauli mbiu ya toleo la 54 la Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu yaKairo

Ali Mahmoud

Dkt. Nevin El-Kilani, Waziri wa Utamaduni, alitangaza kuwa Toleo la 54 la Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu ya Kairo litafanyika pamoja na ufadhili wa Rais Abd El Fattah El-Sisi.

Toleo la 54 litafanyika likiwa na kauli mbiu “Kwa Jina la Misri, pamoja twasoma, twafikiri na twajenga”, na litafanyika kuanzia Januari 25 hadi Februari 6.

Waziri huyo ameeleza kuwa Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu atazindua toleo jipya la maonesho hayo.

Hayo yamejiri wakati wa mkutano na waandishi wa habari, leo, Jumatatu, kutangaza maelezo ya toleo la 54 la Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu ya Kairo, yaliyopangwa kufanyika Januari 25, katika Eneo la Maonesho, kwenye Kituo cha Manara katika The 5th Settlement.

Dkt. Nevin El-Kilani, Waziri wa Utamaduni, Dkt. Ahmed Bahey El-Din, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Umma ya Misri ya Vitabu, Balozi wa Ufalme wa Hashemite wa Yordani jijini Kairo, Balozi Amjad Al-Adaila, nchi ngeni ya heshima, Saeed Abdo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wachapishaji wa Misri, Mohamed Rashad, mwenyekiti wa Shirikisho la Wachapishaji Wa Kiarabu, Hisham Okasha, Mwenyekiti wa Benki ya AlAhly ya Misri, wawakilishi wa kampuni ya muungano ya uchapishaji, uchapishaji na teknolojia ya habari iliyotekelezwa katika jukwaa la maonesho, na wajumbe wa kamati yake ya juu, wote wameshiriki katika tangazo la maelezo ya toleo jipya.

Ufalme wa Hashemite wa Yordani utakuwa mgeni wa heshima katika toleo la 54, na marehemu mbunifu Salah Jahin, mhusika wa maonesho, na mwandishi wa watoto, Kamel Kilani mhusika wa maonesho ya watoto kama mwanzilishi wa fasihi ya watoto sio tu katika Misri bali pia katika Ulimwengu wa Kiarabu.

Back to top button