TAMISEMI SPORTS CLUB ENDELEZENI NIDHAMU KWENYE MICHEZO
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila amewataka wanamichezo wa Timu ya TAMISEMI Sports Club kuendeleza nidhamu, juhudi na ushirikiano katika michezo ya SHIMIWI inatotegemewa kuanza Septemba 28, 2023 Mkoani Iringa
Mhandisi Mativila ameyasema hayo leo Septemba 26, 2023 kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Ndugu Adolf Nduguru Mkoani Dodoma wakati akiiaga Timu hiyo inayoenda kushiriki Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI)
Amewataka kuwa na fikra chanya na kujua uzito wa michezo hiyo na kuwa na nia ya kurudi na ushindi katika michezo yote wanayokwenda kushiriki ambayo ni netiboli, riadha, kuvuta kamba, kuendesha baiskeli na kurusha tufe.
“Nataka muwe na fikra chanya imani kubwa na moyo wa ushirikiano mcheze kama timu msaidiane na mstawishe mshikamano yenu” amesema Mhandisi Mativile