Habari

NDUNGURU AWATAKA MA RAS KUTIMIZA MAONO YA RAIS SAMIA

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Adolph Ndunguru amewataka Makatabu Tawala wa Mikoa wapya kwenda kutimiza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Makatibu Tawala hao ambao wameapishwa leo Ikulu ya Magogoni  ni  RAS wa Mtwara, Bahati Geuzye na RAS Geita Mohamed Gombat.

Akizungumza bara baada ya kukutana na wateule hao na kuwakabidhi nyenzo za kufanyi kazi Bw. Ndunguru aliwataka kwenda kuwajibika ipasavyo na kuwatumikia wananchi.

“Tunamshukuru sana mheshimiwa Rais, Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutuongezea nguvu katika ofisi yetu, hivyo nendeni mkawatumikie wananchi.”

Pia amewataka watendaji hao kwenda kusimamia vyema miradi ya maendeleo, kukusanya mapato ya serikali, kujenga uhusiano na taasisi zingine kuwatumikia wananchi.

“Naamnini wamnakwenda kutumikia serikali vizuri ili nia ya serikali ya awamu ya sita ya kupeleka maendeleo wananchi wake iweze kufikiwa katika mikoa yenu.”

Akizungumza baada ya kukabidhiwa vitendwa kazi Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bahati  amemshukuru Rais Samia kwa kumteua kuwa Katibu Tawala na ameahidi kwenda kusimamia maono ya Mhe. Rais kwa kuhakikisha kuwa Mtwara inafunguka na kupata maendeleo ya kiuchumi.

“Ninahidi kushirikia na watendaji ili twende kuifungua Mtwara kiuchumi na hayo ndio maono ya Rais.”

Naye Katibu Tawala za Mkoa wa Geita Bw. Gombat aaliahidi kwenda kusimamia uadilifu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kushirikiana nao ili kuleta maendeleo ya pamoja ya Mkoa wa Geita

Back to top button