UTT AMIS YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI KWA WAKUU YA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA MIKOA

Katika kipindi cha miaka miwili mfululizo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS Tanzania imepata faida kutoka sh.bilioni 539 hadi sh.trilioni 1.5 sawa na asilimia 185.
Hayo yameelezwa kwenye mafunzo ya Wakuu wa Mikoa yanayofanyika kwneye chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Kibaja mkoani Pwani na Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala, wakati akizungumza viongozi hap.
Migangala amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne mfululizo, Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS Tanzania imepata faida na mtaji unafikia sh.trilioni 1.5 kutoka sh.bilioni 290 zilizopatikana mwaka 2014 hadi 2019.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa kiasi hicho cha faida ni kikubwa na hakijawahi kupatikana tangu kampuni hiyo ianzishwe ambapo lengo la awali la UTT AMIS ilikuwa ni kupata faida kutoka Sh.bilioni 290 hadi 485 kwa kipindi cha miaka mitano.
Amewahamasisha Viongozi kutangaza fursa hiyo kwenye Mikoa yao na pia kaa wao kuwekeza kwenye mifuko mbalimbali inayotolewa na UTT-AMIS.