ZAIDI YA WATAALAM 800 KUJADILI MKATABA WA LISHE DODOMA

Wataalamu zaidi ya 800 kutoka wizara za kisekta, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wa lishe wanatarajiwa kukutana Jijini Dodoma kujadili na kufanya tathimini ya mkataba wa lishe uliosainiwa kati ya Mhe.Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Wakuu wa Mikoa yote nchini.
Ujumbe huo unajumuisha Mawaziri wa Kisekta, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri,Waganga Wakuu wa Mikoa, na Wilaya pamoja na wataalamu wa Afya na Lishe wa Mikoa na Halmashauri.
Mkutano huo utafanyika tarehe 29 Augosti 2023 katika Ukumbi wa jiji uliopo mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma na mgeni rasmi atakuwa waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh.Angelah Kairuki (MB).
Mkataba wa Lishe umekuwa ukitekelezwa nchini Tanzania kwa miaka sita sasa tangu mwaka 2017/18.
Kutokana na hali ya Lishe na udumavu ilivyokuwa kwa watoto chini ya miaka mitano Mhe. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani aliagiza kuwepo kwa Mkataba wa usimamiaji wa shughuli za Lishe baina yake na Wahe. Wakuu wa Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara ili kuhakikisha kuwa suala la Lishe linapewa kipaumbele.