Habari Tofauti
WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2023 KUANZA MASOMO YAO LEO

0:00
Wanafunzi wa Kidato cha tano wapatao 130, 446 wataanza masomo yao leo kwenye shule za Sekondari 548 kati ya hao wanafunzi wa bweni ni 125,402 na wanafunzi 5,044 ni wanafunzi wa kutwa.
Kutokana na ongezeko la wanafunzi wa kidato cha Tano, Serikali ilitoa fedha za kuongezea miundombinu ya mabweni ili kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano ambao wengi wao ni wa shule ya bweni.
Shule za bweni walizopangiwa wanafunzi hawa ni za Kitaifa na wanafunzi hawa wamechanguliwa kutoka mikoa yote Tanzania bara na kupelekwa katika mikoa tofauti tofauti ili kujufunza mazingira mapya, utaifa na kuwa wamoja.