RAIS SAMIA AAGIZA NYUMBA YA PATRON KUJENGWA AZANIA SEKONDARI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angelah Kairuki amesema Mhe. Rais ameagiza nyumba ya mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Azania ijengwe mara moja ili mwalimu huyo awepo wakati wote kusimamia wanafunzi wanaokaa bweni katika shule hiyo.
Waziri Kairuki ametoa kauli hiyo leo wakati alikabidhi magari 10 ya Maafisa Elimu Sekondari yaliyonunuliwa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).
Amesema wakati namuaga Mhe. Rais kuwa leo ntakua Azania Sekondari kwa ajili ya hafla ya ugawaji wa magari akaniambia anafahamu changamoto ya shule hii kuwa hakuna Patron kwa sababu hakuna nyumba ya shule anayoweza kuishi ili kuwa karibu na wanafunzi hao wakati wote hivyo ameelekeza nyumba hiyo ijengwe mara moja’ Kairuki
Ameongeza kuwa kwa maelekezo hayo ya Mhe. Raia nawataatifu kuwa tutaleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo na changamoto zingine tutaendelea kuzitatua kwa kadri fedha inavyooatikana.