Habari Tofauti

HOSPITALI YA WILAYA YA BUKOBA YATAKIWA  KUANZA KUTOA HUDUMA ZA MIONZI NA UPASUAJI

0:00

Hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Bukoba imetakiwa kuanza kutoa huduma ya Mionzi na Upasuaji ifikapo  Septemba 1, 2023

Maelekezo  hayo yametolewa  na Mkurugenzi wa Idara ya Afya,  Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Ntuli Kapologwe  wakati wa kikao cha tahmini na ufuatiliaji kilichofanyika katika Hospitali ya mashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini.

“Hospitali hii imejengwa mwaka 2017 na serikali ya Awamu ya Sita imeshaleta Mashine za Mionzi na vifaa kwa ajili ya Upasuaji kwahiyo hakuna sababu yeyote inavyofanya huduma hizi zisiwepo hapa nawaelekeza kuanza kutoa huduma hiyo mara moja ” amesisitiza Dkt.Ntuli

 Amesema  Hospitali hiyo imegharimu shilingi bilioni 3.1.hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa hakikisha huduma hizo zinaanza kutolewa ifiapo Septemba 1, 2023

 “Naelekeza  ifikapi mwezi Septemba mwaka huu  huduma hizi ziwe zimeanza na unipe taarifa.Nataka ikifika tarehe hiyo nione picha ukiwa umemshika mtoto aliyezaliwa katika chumba hiki Cha upasuaji’ amesisitiza

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera ameahidi kuyafanyia kazi maelekexo hayo na kusema kuwa hadi ifikapo Septemba shughuli  za upasuaji na mionzi zimeanza kutolewa

Vilevile,  Dkt.Kapologwe amesisitiza uwajibikaji wa kiwango cha juu kwa wafanyakazi wote wa sekta ya Afya nchini ili kuweza kutimiza lengo kuu la kutoa huduma bora za afya kwa  wananchi.

“Serikali imeajiri watumishi wapya  wa Afya zaidi ya 24,000 na wengi wenu ni vijana hivyo nawasisitiza kutumia ujuzi wenu vizuri ili tuone matokeo chanya.

Amemtaka  Mganga Mkuu wa wilaya na Mkoa  kuwajengea  uwezo watumishi wapya ili waweze kuendana na Mazingira.

Timu ya tathmini , ufuatiliaji na  usimamizi shirikishi kutoka TAMISEMI ipo katika ziara ya kukagua miradi na ubora wa huduma za chanjo, Lishe na Ustawi wa Jamii Mkoani Kagera.

Back to top button