Habari Tofauti

Balozi wa Misri nchini Senegal ampokea Waziri wa Afya wa Cape Verde

Mervet Sakr

Balozi Khaled Aref alimpokea Filomena Gonaçalves, Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Cape Verde, kando ya ziara yake huko Dakar, ambapo walijadili njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa sekta ya Afya na Dawa.

Wakati wa mkutano huo, Balozi Khaled Aref alikagua juhudi za serikali ya Misri za kuzingatia sekta ya Afya ya binadamu, na kutoa huduma za matibabu zilizojulikana, akibainisha mafanikio ya Misri katika kutokomeza virusi vya C kupitia mpango wa Afya wa milioni 100.

Kwa upande wake, Waziri alipongeza sehemu maalum ambayo Misri inafurahia nchini mwake, ambayo inatokana na Misri kupeleka madaktari huko Cape Verde baada ya uhuru wake mwaka 1975, akiwemo daktari wa upasuaji Maurice Makar, aliyetunukiwa heshima kubwa kwa kutambua kazi yake kwa kujitolea kwa miaka 34 nchini.

Waziri huyo alisema kuwa atashiriki katika “Mkutano wa Dunia wa Idadi ya Watu, Afya na Maendeleo” Septemba ijayo huko Kairo na anatarajia kutembelea Jiji la Dawa na makampuni ya dawa kujadili uwezekano wa ushirikiano katika uwanja huu kwa kuzingatia kuanzishwa kwa sheria mpya nchini mwake kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya dawa.

Back to top button