Uchumi

Rais El-Sisi afuatilia kwa makini Viashirio vya kiuchumi vya Misri

Tasnem Muhammad

Jumapili Agosti 6, Rais Abdel Fattah El-Sisi alifanya mkutano na Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly, Gavana wa Benki Kuu ya Misri Hassan Abdullah, Mkuu wa Upelelezi Mkuu Meja Jenerali Abbas Kamel, Waziri wa Mipango na Maendeleo ya Uchumi Dkt. Hala Al-Saeed, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Dkt.Rania Al-Mashat, Waziri wa Fedha Dkt. Mohamed Maait, na Mshauri wa Rais wa Masuala ya Fedha Meja Jenerali Mohamed Amin.

Msemaji rasmi wa Ofisi ya Rais wa Misri, Mshauri Ahmed Fahmy, alisema kuwa mkutano huo ulipitia viashirio vya uchumi wa Misri na maendeleo ya hivi karibuni katika hali ya uchumi wa Dunia, kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika ngazi ya kimataifa, inayoweka athari za kiuchumi kwa uchumi mbalimbali wa Dunia, ikiwa ni pamoja na Misri, ambapo hatua kubwa zilizochukuliwa katika kipindi cha mwisho ziliwasilishwa ili kuendelea kuboresha viashiria vya jumla vya uchumi na kuvutia uwekezaji tofauti. Katika muktadha huo huo, Rais aliarifiwa juu ya malengo maarufu ya kiuchumi katika awamu inayofuata, na juhudi za ushirikiano na taasisi mbalimbali za kifedha za kimataifa kuendelea kutekeleza mchakato wa mageuzi ya kiuchumi.

Msemaji huyo aliongeza kuwa Rais alisisitiza wakati wa mkutano huo kuendelea kuweka juhudi za hali ya juu ili kupunguza athari za mgogoro huo kwa wananchi, kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei, kuendelea kutekeleza mageuzi ya kimuundo, na kuongeza nafasi ya sekta binafsi, hasa kwa kuondoa vikwazo vya urasimu, na kufikia kanuni ya kutokuwa na upande wowote, kwa njia inayosaidia kujenga mazingira ya kuvutia kwa uwekezaji zaidi wa ndani na nje, na kuongeza mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali, kwa njia inayosaidia uchumi wa kitaifa na kuinua viwango vya mapato ya wananchi.

Back to top button