Habari Tofauti

Viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Njombe wameshiriki semina ya maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 (TDV 2050)

Semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango, imefanyika Julai 19,2023 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe ikilenga kutangaza,kutoa elimu,kuhamasisha na kuiandaa jamii  kushiriki zoezi la kukukusanya maoni kwa ajili ya kuandaa dira ya taifa ya maendeleo kwa miaka 25 ijayo kuanzia mwaka 2025 hadi 2050.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya uandishi wa dira ya 2050 Dkt Rosemary Taylor kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam amesema, semina iliyofanyika kwa viongozi na wadau mbalimbali ni mojawapo ya hatua za awali kwenye maandalizi ambayo itasaidia kufikisha taarifa kwa jamii ili kila mtanzania aweze kujiandaa kushirki zoezi la kutoa maoni.

Baadhi ya viongozi walioshiriki semina hiyo, Anna Mwalongo ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Njombe na Joram Hongoli Mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Njombe wamesema,dira ya maendeleo ya taifa ina mgusa kila mwananchi na kwa kuwa zoezi la uandaaji wa dira 2050 ni shirikishi, wao kama viongozi watashirikiana kwenye kuhamasisha na kuwaanda wananchi kushiriki kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao ili kupata dira ambayo itasaidia kutoa majibu ya changamoto mbalimbali kwenye jamii.

Pamoja na Kukaribia kwa ukomo wa dira ya taifa ya maendeleo 2025 iliyofanikisha kuingiza Tanzania katika kundi la nchi zenye hadhi ya uchumi wa kipato cha kati, madhumuni mengine ya kuandaa dira ya taifa ya maendeleo kwa miaka 25 ijayo kuanzia 2025 hadi 2050 ni ili kuwa na mipango na vipaumbele vya muda mrefu,Mabadiliko ya  mazingira na matakwa ya wananchi kimaendeleo, Kuendeleza Mafanikio na malengo ya Dira 2025 na Umuhimu wa Taifa kuwa na mwelekeo.

Kaulimbiu ya maandalizi ya zoezi la ukusanyaji wa maoni inasema “Shiriki Katika Kuijenga Tanzania Tuitakayo Ifikapo 2050”

Back to top button