Habari Tofauti

Waziri wa Makazi apokea mwaliko wa mwenzake wa Angola kutembelea Angola ili kuimarisha ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja

Zeinab Makaty

Dkt. Assem El-Gazzar, Waziri wa Makazi, Huduma na Jumuiya za Mijini, alipokea mwaliko kutoka kwa Bw. Carlos Alberto Dosanto, Waziri wa Ujenzi wa Umma, Miji na Makazi nchini Angola, kutembelea Angola, kujibu ziara ya Waziri wa Angola mjini Kairo, na kuimarisha ushirikiano katika nyanja zenye maslahi ya pamoja, hivyo wakati wa mkutano wake na Balozi Nelson Manuel Cosme, Balozi wa Angola mjini Kairo.

Dkt. Assem El-Gazzar amekaribisha mwaliko wa mwenzake wa Angola kwa ziara ya kikazi katika Angola, kuimarisha mahusiano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kuhamisha uzoefu wa Misri kwa ndugu zetu nchini Angola katika nyanja zilizoelezwa na balozi wa Angola, ikiwa ni pamoja na, kuanzishwa kwa miji mipya, ambayo ni mji mkuu mpya wa utawala, miradi ya miundombinu (maji ya kunywa na usafi wa mazingira),  miradi ya makazi ya aina mbalimbali, miradi ya barabara na madaraja, na nyanja zingine za maendeleo ya miji.

Waziri huyo wa Makazi alisisitiza kuwa makampuni ya kikandarasi ya Misri, yawe ni kampuni binafsi au za umma, ambazo kwanza ni Kampuni ya Arab Contractors (yatekeleza miradi mbalimbali kwa ndugu zetu katika nchi za Afrika, ambayo kubwa ni mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere na Kituo cha Umeme Tanzania), wako na uzoefu mkubwa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya miji, katika uwezo wa makada wa binadamu, ukubwa wa vifaa na kazi iliyofunzwa kwa kiwango cha juu, pamoja na wazalishaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi, akifafanua kuwa idadi ya makampuni yanayofanya kazi katika miradi mbalimbali katika kiwango cha Jamhuri imefikia makampuni takribani 3,000 na sasa makampuni hayo yakawa na uwezo wa kutekeleza miradi mbalimbali nje ya nchi ya Misri hasa kwa ndugu zetu wa Afrika.

Balozi wa Angola mjini Kairo ameelezea shukrani zake kwa ziara ya Rais wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi nchini Angola, iliyofungua mlango wa ziara za ngazi ya juu zaidi za maafisa wa Misri, na ziara ya Waziri wa Nyumba itakuwa ufunguzi wa ziara hizo, kwa ushirikiano katika sekta ya ujenzi, ambayo ni moja ya sekta muhimu kwa Angola.

Balozi Nelson Manuel Cosme, Balozi wa Angola mjini Kairo, aliwasilisha rasimu mpya ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara za makazi za Misri na Angola, akieleza kuwa mkataba huo unaweza kusainiwa wakati wa ziara ya Dkt. Assem El-Gazzar nchini Angola.

Back to top button