Habari

Mjumbe wa Rais Putin katika Mashariki ya Kati na Afrika akaribisha Mkutano wa kilele wa Kairo kwa nchi jirani za Sudan

Mervet Sakr

Balozi Nazih Nagari, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mjini Moscow, alikutana na Bw. Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na Mjumbe Maalum wa Rais Putin kwa Mashariki ya Kati na Afrika.

Mkutano huo ulijadili maandalizi yanayoendelea kwa ajili ya Mkutano wa Urusi na Afrika, ambao utaandaliwa na mji wa Urusi wa St. Petersburg Julai 27 na 28.

Pia walijadili maendeleo nchini Sudan, ambapo Bogdanov alikaribisha juhudi za Misri katika suala hilo, haswa matokeo ya mkutano wa kilele wa nchi jirani za Sudan uliofanyika Kairo mnamo Julai 13, wakiwa na matumaini ya kurejesha Amani na Utulivu nchini Sudan.

Mkutano huo pia uligusia masuala mengine kadhaa katika kanda hiyo, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya Palestina na Libya, ndani ya muktadha wa uratibu uliopo kati ya nchi hizo mbili juu ya masuala mbalimbali ya kikanda.

Back to top button