DKT. MSONDE ASISITIZA MATUMIZI YA VISHIKWAMBI KWA WALIMU

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde amewataka Maafisa Elimu Kata kuwasimamia na kuwasidia Walimu namna kutumia vishikwambi walivyopewa kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua ubora wa elimu nchini.
Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo wakati akifunga Mafunzo endelevu ya walimu kazini (MEWAKA) kwa Maafisa elimu kata 1,209 yaliyofanyika katika chuo cha Ualimu Klerruu mkoani Iringa.

Dkt. Msonde amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha utendaji kazi wa walimu nchini kwa kuwatekelezea masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapatia walimu vishikwambi hivyo ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji.
“Kupitia mafunzo haya ya MEWAKA mmefundishwa namna mnavyopaswa kutumia vishikwambi katika ufundishaji na ujifunzaji, hivyo nitoe rai kwenu kuhakikisha vinatumika ipasavyo kuinua ubora wa Elimu nchini”

Amewataka kutumia vishikwambi hivyo kuingia katika Maktaba Mtandao na Mfumo wa Kujifunza (LMS) wa Taasisi ya Elimu Tanzania ili kujipatia vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na mbinu mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji.
Aidha, Dkt. Msonde amewata Maafisa Elimu Kata kusimamia kikamilifu vituo vya walimu na kuvitumia kuendesha mafunzo ya walimu kazini ili kuimarisha ufundishaji na ufundishaji.
“Kupitia mafunzo haya mtayafahamu vema majukumu yenu hivyo kahakikisheni vituo vya walimu vinatumika kuendesha mafunzo ya walimu kazini kama ilivyokusudiwa” Dkt. Msonde amesisitiza.
Aidha, amewata Maafisa Elimu Kata kuwa chachu ya kuendeleza na kusimamia Mafunzo Endelevu ya Waalimu Kazini (MEWAKA) ili kuboresha ujifunzaji kwa wanafunzi wa Elimu Awali na Msingi.
Amesema katika mwaka huu wa fedha 2023/24 Serikali imejipanga kuendelea kutoa mafunzo kazini yatakayoimarisha ufundishaji na ufunzaji na itaendelea kuimarisha utoaji wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini kwa njia ya TEHAMA. Naye, Mratibu wa Mafunzo kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekn.










