Waziri Mkuu afuatilia na Waziri wa Umwagiliaji matokeo ya ziara yake katika nchi kadhaa za Bonde la Mto Nile
Mervet Sakr

Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, amefanya mkutano leo na Dkt. Hany Swailem, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, kujadili matokeo ya ziara yake katika nchi kadhaa za Bonde la Mto Nile.
Waziri Mkuu alianza mkutano huo kwa kusisitiza nia kubwa ya Misri katika kuwasaidia ndugu zake katika nchi za Bonde la Mto Nile, na kutoa misaada mbalimbali ya kiufundi, ili kuimarisha ushirikiano na nchi hizo, katika kutekeleza maagizo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kuzingatia kukidhi mahitaji ya nchi ndugu na rafiki za msaada wa kiufundi na utaalamu mbalimbali, ili kuziwezesha nchi hizo kusimamia vizuri rasilimali zao za maji na kushughulikia matatizo yoyote wanayoweza kukabiliana nayo katika uwanja huo.
Katika mkutano huo, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji aliwasilisha matokeo ya ziara zake mnamo siku zilizopita kwa nchi sita za Bonde la Mto Nile, ambazo ni Sudan, Sudan Kusini, Kenya, Burundi, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akieleza kuwa alikuwa makini wakati wa ziara hiyo ili kubaini mahitaji ya nchi hizo rafiki za msaada wa kiufundi katika nyanja ya usimamizi wa rasilimali za maji, na nini Misri inaweza kuchangia katika nchi hizo.
Waziri huyo pia alipitia matokeo ya mazungumzo yake na mawaziri na maafisa wa serikali, pamoja na wabunge kadhaa, katika nchi alizotembelea na kuongeza kuwa kuna maandalizi ya kutembelea nchi nyingine kutoka Bonde la Mto Nile mnamo kipindi kijacho, na mifumo kadhaa ya ushirikiano na Misri itaanzishwa.