Habari Tofauti

Mwenyekiti wa Arab Contractors atembelea miradi ya kampuni hiyo nchini Uganda

Ali Mahmoud

Katika mfumo wa ufuatiliaji wake kwa miradi nje ya nchi, Mhandisi Sayed Farouk, Mwenyekiti wa Kampuni ya Arab Contractors , alitembelea nchi ya Uganda wakati ambapo alikagua miradi inayoendelea kujengwa, nayo ni mradi wa Chuo kikuu Cha Aga Khan katika Mji mkuu wa Uganda Kampala, ambao kampuni hiyo ilishinda hivi karibuni na una jengo la kitaaluma, linalojumuisha ghorofa ya chini na sakafu 6 za kawaida, na jengo la makazi linalojumuisha ghorofa ya chini na sakafu nane.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo pia alitembelea Mradi wa Barabara na Daraja la Saka, unaojumuisha barabara inayopita kwenye kinamasi chenye maji mengi chenye urefu wa kilomita 4.5 na daraja linalovuka Mto Ambulugoma.

Wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi aliambatana na Mhandisi.Mohammed Talba, Mwanachama Mtendaji wa Kampuni ya Arab Contractors ya Uganda, na Bw. Emad Obaid, msimamizi wa fedha wa sekta ya Afrika.

Mwishoni mwa ziara hiyo, Mwenyekiti aliwashukuru wafanyakazi wote wa Misri na Uganda kwa juhudi walizozifanya na ubora wa juu wa miradi hiyo.

Inatajwa kwamba Kampuni ya Arab Contractors ya Uganda, hivi karibuni, ilipata cheti cha kampuni bora ya kimataifa ya ukandarasi yenye maoni ya mustakabali katika nyanja za ujenzi na makazi kwa mwaka wa tano mfululizo, kutokana na michango ya kampuni kufikia matarajio na maoni ya Uganda 2040.

 

Back to top button