Mabingwa wa Hockey wa Al-Sharqiya waandika historia na wakawa wakuu wa mchezo huo katika Barani Afrika
Ali Mahmoud
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Dkt. Mamdouh Ghorab, Gavana wa mkoa wa Al-Sharqiya, Jumatatu Asubuhi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kairo,wamepokea ujumbe wa timu ya mpira wa Hockey ya “Wanaume” ya Klabu ya Michezo ya Al-Sharqiya, baada ya kushinda mechi ya fainali katika michuano ya Afrika ya klabu za mabingwa, iliyofanyika Nairobi, Mji Mkuu wa Kenya, na ilishinda nafasi ya kwanza dhidi ya timu ya ExCheckers ya Ghana, ambayo ilimalizika kwa matokeo ya 4-2 kwa Timu ya Al-Sharqiya, kwa mahudhurio ya mbunge Ahmed Abdul-Gawad, mwanachama wa Seneti na Naibu Mwenyekiti wa chama cha Mostaqbal Watan, na kundi la waheshimiwa manaibu wa Mkoa wa Al-Sharqiya.
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliipongeza bodi ya wakurugenzi ya Klabu ya Michezo ya Al-Sharqiya, wachezaji wa timu ya mpira wa Hockey kwenye klabu, na wafanyikazi wa kiufundi na kiutawala kwa kushinda taji la Ubingwa wa Afrika.
Waziri huyo alitathmini mafanikio ya kihistoria ya Timu ya Hockey ya Al-Sharqiya, ambapo ikawa mmiliki wa taji la kihistoria la ubingwa, na ilirekodiwa katika Rekodi za Dunia za Guinness kwa kushinda Ubingwa wa Afrika mara 26 kutoka Jumla ya mashindano 32 ya Kiafrika, pamoja na ushindi wa timu kwa Ligi, Kombe na Ubingwa bora katika ngazi ya ndani.
Dkt. Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo yafanya kazi kusaidia mashirikisho yote ya michezo, na inaandaa mpango kamili kwa ajili ya Olimpiki ya Paris 2024, ili Mabingwa wa Misri waweze kuendelea kufikia mafanikio yao.
Waziri aliashiria kuwa Serikali ya Misri daima huwaunga mkono wachezaji wake na yawapa msaada muhimu, ili kuwaandaa vizuri kushinda ubingwa na medali.
Kwa upande wake, bodi ya wakurugenzi ya Klabu ya Michezo ya Al-Sharqiya, ikiongozwa na Dkt. Hamdi Marzouk, Mwenyekiti, wajumbe wa bodi, wafanyakazi wa kiufundi na kiutawala wa timu na wachezaji, walitoa pongezi kwa shukrani na kutathmini kwa Waziri wa Vijana na Michezo, Dkt. Ashraf Sobhy, kwa uangalizi wake na ufuatiliaji wa hali za timu moja kwa moja wakati wa mashindano.