Habari

Waziri wa Umwagiliaji wa Misri ajadiliana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Kenya njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo mbili ndugu

Mervet Sakr

Wakati wa ziara yake huko nchi ndugu ya Kenya. Prof.Hany Swailem, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, alikutana na Bi. Alice Mutuni Wahumi, Waziri wa Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji wa Kenya, kwa mahudhurio ya Balozi Wael Attia, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Kenya, ujumbe rasmi ulioandamana na Waziri, wawakilishi wa Ubalozi wa Misri na maafisa wakuu wa Kenya.
Katika mkutano huo, mawaziri hao wawili walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika uwanja wa rasilimali za maji na umwagiliaji kati ya nchi hizo mbili ndugu.

Dkt. Swailem alielezea furaha na shukrani zake kwa kukutana na Bi. Wahomi, akisisitiza azma yake ya kufanya kazi pamoja ili kuimarisha vifungo vya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa Maendeleo endelevu ya rasilimali za maji, na akisisitiza nguvu ya mahusiano ya kimkakati kati ya Misri na Kenya katika ngazi zote, na nia ya Misri ya kuimarisha ushirikiano huo kabisa ndani ya muktadha wa nia ya kuunga mkono vifungo vya ushirikiano kati ya Misri na nchi za Bonde la Mto Nile kwa kujenga maslahi ya pamoja na kufikia manufaa ya pande zote.

Pia aliashiria nyuma kwa historia ya ushirikiano wa kiufundi uliozaa matunda kati ya Misri na Kenya, ambao ni mfano wa kufuatwa kwa mahusiano ya pande mbili kwa kuzingatia misingi ya ushirikiano na mahusiano mzuri, kwani ushirikiano huo ulianza mnamo 1993 na utoaji wa msaada wa kiufundi wa Misri kwa Kenya katika uwanja wa maji chini ya ardhi kupitia mkataba wa makubaliano uliotiwa saini kati ya nchi hizo mbili kutoa msaada kwa Kenya kuchimba visima 180 vya chini ya ardhi.

Pia Mkataba wa makubaliano ulitiwa saini mwaka 2016 kutekeleza mradi wa kuendeleza na kusimamia rasilimali za maji, unaojumuisha shughuli mbalimbali za kuongeza matumizi bora ya rasilimali za maji na kujenga uwezo katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na (kuchimba visima vya chini ya ardhi – kuanzisha mabwawa ya kuvuna maji ya mvua – mafunzo na kujenga uwezo katika maeneo mbalimbali ya usimamizi wa rasilimali za maji – matumizi ya mifumo ya kisasa ya umwagiliaji katika nyanja ya kilimo), na ziara iliandaliwa hapo awali kwa wataalam wa Misri nchini Kenya, wakati ambapo mipango ya utekelezaji wa mradi iliandaliwa na kuidhinishwa na pande zote mbili.

Dkt. Swailem alisisitiza nia yake ya kuamsha miradi ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kwa kuzingatia Mpango wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi katika Sekta ya Maji, ambayo Misri iliizindua katika mkutano uliopita wa hali ya hewa, unaolenga kutekeleza miradi katika uwanja wa kukabiliana na mabadiliko katika nchi za Afrika kwa mara ya kwanza, pamoja na jitihada za Misri za kukaribisha na jitihada za mara kwa mara za kuimarisha ushirikiano wa kiufundi, kubadilishana uzoefu na kujenga uwezo na nchi mbalimbali za Afrika, hasa kwa utayari wa Misri kuwa kituo cha Afrika cha kujenga uwezo katika uwanja wa kukabiliana na mabadiliko pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Pia alisisitiza kuwa Misri itajitahidi wakati wa urais wake wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCAO) mnamo miaka ya 2023 na 2024 ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi mbalimbali za Afrika katika ngazi ya bara ili kukabiliana na changamoto za maji.

Back to top button