Habari Tofauti

Misri yatuma misaada haraka ya matibabu kwa Uturuki, Syria ili kukabiliana na athari za tetemeko kubwa la ardhi katika nchi hizo mbili 

Mervet Sakr

0:00

Katika kutekeleza maagizo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri na Kamanda Mkuu wa Majeshi, kuwasaidia watu wa Uturuki na Syria katika shida zao na kuwasaidia kupunguza athari za tetemeko kubwa la ardhi katika nchi hizo mbili, lililosababisha athari za uharibifu mkubwa pamoja na idadi kubwa ya waathirika na majeruhi.

Ndege tano za uchukuzi wa kijeshi zilipaa kutoka kambi ya anga ya Kairo Mashariki zikiwa zimesheheni kiasi kikubwa cha dawa na vifaa tiba vilivyotolewa na Wizara ya Afya na Idadi ya Watu kwa watu wa nchi hizo mbili ili kuwasaidia kupunguza athari za tetemeko kubwa la ardhi.

Maafisa wa nchi hizo mbili wameelezea kutathmini kwao na juhudi na misaada ya Misri iliyotolewa na serikali ya Misri ;kudhibiti hali hiyo mbaya kutokana na tetemeko hilo kubwa la ardhi.

Misaada ya Misri inayotolewa kwa pande za Uturuki na Syria ni uthibitisho wa umuhimu wa msaada wa kibinadamu kukabiliana na ajali za matukio ya asili, yanayochangia kusaidia mahusiano ya kutegemeana na undugu kati ya watu ili kushinda shida.

Back to top button