Habari Tofauti

Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri afanya kikao cha mazungumzo ya mwisho na mwenzake wa Burundi

Mervet Sakr

0:00

Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri afanya kikao cha mazungumzo ya mwisho na mwenzake wa Burundi kujadili njia za kuimarisha ushirikiano katika uwanja wa usimamizi jumuishi wa rasilimali za maji

Kikao cha mazungumzo ya mwisho kilifanyika kati ya Prof.Hany Swailem, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, na Bw. Sanctus Niragera, Waziri wa Mazingira, Kilimo na Mifugo wa Taifa la Burundi, kwa mahudhurio ya Balozi Yasser Al-Atwi, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Burundi, na wataalamu na mafundi kutoka pande zote mbili, kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika uwanja wa usimamizi wa rasilimali jumuishi za maji, ndani ya muktadha wa kufuata msimamo wa itifaki ya ushirikiano wa pamoja iliyosainiwa Machi 2021.

Wakati wa majadiliano hayo, Dkt. Sweilam alisisitiza dhamira ya Misri ya kuimarisha uhusiano wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali, haswa rasilimali za maji na umwagiliaji, akielezea msaada wa Misri kwa sera za maendeleo zinazotekelezwa na Taifa la Burundi, zinazolenga kuongeza viwango vya maendeleo ya kilimo na kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

Mheshimiwa alifafanua kuwa Misri imedhamiria kukamilisha tafiti mbalimbali za mabwawa ya kuvuna maji ya mvua, ambapo miradi ya kilimo itajengwa ili kukidhi mahitaji ya upande wa Burundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia alisisitiza umuhimu wa kubadilishana uzoefu na ziara baina ya nchi hizo mbili ndugu ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji na kufikia matumizi bora ya rasilimali za maji zilizopo, akigusia mwendelezo wa upande wa Misri katika kuhamisha uzoefu na kujenga uwezo kwa makada wa Burundi kupitia kozi mbalimbali za mafunzo zilizoandaliwa na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Misri na Wizara na taasisi nyingine za Misri.

Kwa upande wake, Waziri wa Burundi alieleza furaha yake kwa ziara hii muhimu ya Waziri wa Umwagiliaji wa Misri huko Burundi, na matarajio yake ya kuendelea na uratibu kati ya pande hizo mbili katika masuala na mada mbalimbali, na kuimarisha mawasiliano na upande wa Misri ili kunufaika na uzoefu wa Misri katika nyanja ya maendeleo ya umwagiliaji na mitambo ya kisasa ya kilimo.

Back to top button