Habari Tofauti

Al-Azhar yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Binadamu

Ali Mahmoud

Al-Azhar Al-Shareif iliandaa sherehe kubwa, katika banda lake katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo, katika toleo lake la 54, kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Udugu wa kibinadamu, Leo, Jumamosi ambayo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Desemba 21, 2020 iwe kumbukumbu ya kutiwa saini kwa hati ya udugu wa kibinadamu kwenye Februari 4; siku ya udugu wa kibinadamu, kama njia ya kukuza zaidi ya uvumilivu, udugu na amani.

Banda la Al-Azhar liliwasilisha sherehe kubwa mnamo saa saba na nusu kamili juu ya hati ya udugu wa binadamu, pomoja na kichwa cha “Dini na Mazungumzo kwa ajili ya Kuishi Pamoja na Amani”, pia sekta ya Taasisi za Azhar inashiriki kwa hati za utangulizi juu ya umuhimu na malengo ya hati, maonesho ya maigizo, ya kisanaa na nyimbo, pamoja na machapisho kwenye hati ya udugu wa binadamu kwenye duka la vitabu, na Gazeti la Noor linashiriki kwa mashindano ya kutambulisha hati, pia itaoneshwa filamu ya maandishi juu ya Sheikh wa Al-Azhar na Papa wa Vatican kuonesha juhudi zao katika njia ya amani, ikiwa ni pamoja na kutiwa saini kwa udugu wa binadamu, inavyoonekana kwenye skrini kuu na Panorama Al-Azhar.

Kwa mwaka wa saba mfululizo, Al-Azhar Al-Shareif yashiriki katika banda maalum katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo katika toleo lake la 54, kulingana na jukumu la elimu na utetezi la Al-Azhar katika kueneza mawazo ya Kiislamu ya wastani ambayo limepitisha kwa zaidi ya miaka elfu moja.

Banda la Al-Azhar kwenye Maonesho hayo lipo katika Ukumbi wa Heritage Na. “4”, na linaenea juu ya eneo la mita elfu moja, linalojumuisha kona kadhaa, kama vile ukumbi wa semina, kona ya fatwa, kona ya hati ya kiarabu, pamoja na kona ya watoto na maandishi.

 

Back to top button