Kituo cha Al-Azhar chashiriki katika shughuli za warsha kuhusu mashirika ya kigaidi Barani Afrika
Ali Mahmoud

Wakati wa ushiriki wake katika shughuli za siku ya kwanza ya warsha iliyofanyika pamoja na kichwa “Mazoea Mema katika taratibu za Uchunguzi wa Uhalifu wa Kigaidi” kutoka Januari 15 hadi Januari 19, 2023, katika Taasisi ya Tafiti na Mazoezi ya Jinai ya Mashtaka ya Umma huko Kairo, kwa ushiriki wa zaidi ya nchi 15 za kiafrika, Dkt. Ehab Shawky El-Sayed, Msimamizi wa Kitengo cha Lugha za Kiafrika katika Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na Misimamo Mikali, alitoa mhadhara wa kutambulisha jukumu la kituo hicho katika kufuatilia mienendo ya mashirika ya kigaidi ulimwenguni kote na kukabiliana na hotuba ya chuki.
“Shawki” alisisitiza kuwa, kukabiliana na ugaidi Barani Afrika kunahitaji mikakati mipya katika nchi zake nyingi haswa zile zenye matatizo ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi ili kupunguza matukio ya vitendo vya kigaidi, pamoja na umuhimu wa kuongeza ufahamu wa kidini kwa vijana wa Afrika ili wasianguke mawindo kwenye mashirika hayo.
Msimamizi huyo wa Kitengo cha Lugha za Kiafrika aliashiria kwamba mashirika ya kigaidi Barani Afrika kwa sasa, haswa katika eneo la pwani, yanaeneza migogoro kati yao kufikia nguvu, utawala na kupata vyanzo vya ufadhili, ambayo ni ushahidi wa uwongo wa mawazo yao na malengo na umbali wao kutoka kwa sheria ya Kiislamu ambayo wanadai kuyatekeleza. Pia alisisitiza umuhimu wa kurejea kwenye vyanzo vinavyotegemeka kupata taarifa, bila kutegemea mitandao ya kijamii kutafuta ukweli.
Inatajwa kwamba warsha hiyo inalenga kuongeza ufahamu kwa kundi kubwa la mashirika ya mahakama, mashtaka na polisi katika nchi za kiafrika na kuwapa mafunzo ya kukabiliana na majaribio yoyote ya kiakili yanayoenezwa na mashirika ya kigaidi, ili kusaidia kuimarisha usalama na utulivu wa jamii na kufikia malengo ya maendeleo ya kina.