Uchumi

Misri: Waziri wa Mipango na Maendeleo ya Uchumi akutana na Waziri wa Nchi katika Kansela ya Shirikisho ya Ujerumani

Ali Mahmoud

0:00

Dkt. Hala Al-Said, Waziri wa Mipango na Maendeleo ya Uchumi, alikutana na Dkt. Joerg Kokez, Waziri wa Nchi katika Kansela ya Shirikisho ya Ujerumani, kujadili njia za ushirikiano katika nyanja za uchumi, miundombinu, nishati na hidrojeni ya kijani, na hivyo wakati wa kushiriki katika kazi za Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos.

Mkutano huo ulijumuisha kubadilishana maoni kuhusu hali za kiuchumi Duniani, pamoja na kujadili njia za Ujerumani kusaidia utalii nchini Misri kutokana na uzoefu wake wenye mafanikio kabla ya kipindi cha machafuko ya kimataifa. pia wamejadiliana kuhusu njia za ushirikiano kwa kuzingatia hali zinazopita ulimwenguni sasa.

Wakati wa mkutano huo, Dkt. Hala Al-Said alishughulikia kuzungumzia hitaji la dharura la dunia kugeukia uchumi wa kijani na kuelekea kwa nishati mbadala, akisisitiza maslahi ya Misri katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa ndani ya mfumo wa juhudi zake za kufikia maendeleo ya kina na endelevu, akiashiria kuwa Misri ilizindua viwango vya uendelevu wa mazingira na kutoa vifungo vya kijani na iwe nchi ya kwanza Barani Afrika kuvizindua. Mbali na mwelekeo wa serikali kupitia Mfuko huru wa uwekezaji kuwekeza katika miradi kadhaa katika sekta mbalimbali, ya maarufu zaidi ni hidrojeni ya kijani, usafirishaji safi, uondoaji chumvi katika maji, nishati mpya na mbadala, na miradi katika sekta za kipaumbele kama vile uzalishaji wa hidrojeni ya kijani, usafirishaji endelevu na miradi yenye ufanisi wa juu katika matumizi ya nishati.

Al-Said pia alizitaja juhudi za serikali katika uwanja wa utalii kama moja ya vyanzo vikuu vya fedha za kigeni, akiashiria jitihada za serikali kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya watalii na mapato yao kwa viwango visivyo na kifani, viwango ambavyo nchi kama Misri inastahili.

Ziara ya Waziri huyo mjini Davos, Uswisi, ilishuhudia kufanyika kwa mikutano kadhaa ya nchi hizo na pia mawaziri wa kimataifa, pamoja na Wakurugenzi Wakuu wa makampuni na taasisi kubwa kujadili nafasi za kuvutia uwekezaji nchini Misri na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali mbalimbali, na pia ushiriki wa sekta binafsi ya kimataifa.

Back to top button