Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua jengo la dharura kwenye hospitali ya Wilaya ya Ruangwa
Ahmed Hassan
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua jengo la dharura kwenye hospitali ya Wilaya ya Ruangwa ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 390.7
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Salvio Wikesi amesema sehemu ya fedha za ujenzi wa jengo hilo ambazo ni shilingi milioni 300 zimetokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mkuu amewataka Wananchi kuwa walinzi wa miundombinu na vifaa tiba vilivyonunuliwa ili waendelee kupata huduma bora na za uhakika.
Pamoja ukamilishaji wa Jengo hilo, pia Rais Dkt. Samia alitoa vifaa tiba vya kisasa, pia Wizara ya Afya ilileta mashine ya xray, mashine ya kutakasia vifaa kabla ya kufanya upasuaji, mashine ya kumfanya uangalizi mgonjwa wakati wa upasuaji