Waziri wa Vijana akutana na kundi la vijana wenye ushawishi kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii
Ali Mahmoud
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na kundi la vijana wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii, ambao walishiriki katika mashindano ya “Kituo cha Wabunifu”, ambayo yalifanywa na wizara kwa kushirikiana na Jukwaa la TikTok.
Waziri huyo akisikiliza maoni ya vijana walioshiriki katika mkutano huo, ambapo faida za shindano la “Kituo cha Wabunifu” kwani vijana hawa wana akaunti rasmi zilizothibitishwa kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii ambayo wanatafuta kupitia kwake kutoa maudhui yenye maana ili kuongeza uelewa wa vijana katika mada mbalimbali.
Waziri wa Vijana na Michezo alieleza uangalifu wa Wizara hiyo kwa kuwaunganisha Vijana wenye ushawishi katika shughuli na mipango mbalimbali inayotolewa na wizara hiyo, na kufikia idadi kubwa ya vijana katika ngazi ya Jamhuri kupitia kuonesha juhudi za wizara na jukumu lake katika kuongeza uelewa kupitia vijana hao.
Waziri huyo aliwatakia heri dhati kwa vijana wanaoshiriki katika Kituo cha Wabunifu, na kuzoeza kwa njia bora katika jitihada za kuwawezesha kutoa maudhui yenye lengo la kuongeza uelewa kwa vijana kupitia wafuasi wao kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii.
Wizara ya Vijana na Michezo imesaini makubaliano ya ushirikiano na jukwaa la “TikTok” kuzindua Programu ya TikTok Creator Hub, kwa lengo la kuwasaidia vijana kujenga ustadi na ujuzi sahihi wa kutumia mitandao ya kijamii, kuongeza ufahamu wa masuala yanayohusu jamii, na kuweka mawazo na kubuni ufumbuzi wa masuala ya umma.
Mashindano ya Kituo cha Wabunifu yalizinduliwa kupitia jukwaa la ”TikTok”, ambapo idadi kubwa ya washiriki walipokelewa, na walichujwa kwenye washiriki 40, na wizara iliandaa warsha ya kuwasaidia vijana kujenga ujuzi, na njia za kutumia mitandao ya kijamii kuongeza uelewa wa masuala ya jamii, kwa mahudhurio ya wasimamizi wa jukwaa, na idadi ya washawishi kwenye mitandao ya kijamii.
Sherehe ya kufunga ilifanyika Novemba iliyopita kutangaza washindi watano ambao waliwasilisha mawazo na ufumbuzi wa ubunifu wakati Misri ilikaribisha kikao cha 27 cha Mkutano wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa.