Habari

Rais El-Sisi: Watu wa Misri wanathibitisha kila siku kwamba mizizi yao ya kina yawachochea kuchukua hatua imara kuelekea siku zijazo

Ali Mahmoud

Rais Abdel Fattah El-Sisi alisema: ninatoa salamu zangu za Shukrani na fahari kwa Watu wote wa Misri, akiashiria kuwa watu wa Misri wanathibitisha kila siku kwamba mizizi yao ya kina inawachochea kuchukua hatua imara kuelekea siku zijazo.

Hiyo ilitokea wakati wa hotuba ya Rais Abdel Fattah El-Sisi pembezoni mwa ufunguzi wa miradi kadhaa katika Mkoa wa Sohag.

Rais alisisitiza kuwa mikono ya Wamisri ina uwezo wa kugeuza ndoto kuwa ukweli.

Aliendelea: maagizo yangu yalikuwa wazi kwa mashirika yote ya serikali kuweka maendeleo ya Misri ya mbele ya vipaumbele.

Leo, Alhamisi, Rais El-Sisi alikagua miradi ya maisha Bora katika kijiji cha Om Douma huko Sohag.

Watu wa Kijiji cha Om Douma walimpokea Rais El-Sisi kwa makofi na vigelegele kabla ya kula kifungua kinywa wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Mkoa wa Sohag.

Mkoa wa sohag umeshuhudia ongezeko kubwa mnamo kipindi cha miaka 8 iliyopita kupitia miradi mikubwa, ambapo jumla ya miradi katika Sohag tangu 2014 hadi sasa, ndani ya mpango wa serikali wa maendeleo ya jumla katika mikoa ya Jamhuri, imefikia miradi 415.

Back to top button