Vijana Na Michezo

“Vijana na Michezo”: Misri yajiandaa kupokea mashindano 3 ya kimataifa yaTaekwondo Februari ijayo

Mervet Sakr

Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy, ilitangaza kuwa Misri itakuwa mwenyeji wa mashindano matatu ya kimataifa ya Taekwondo Februari ijayo, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Taekwondo la Misri, nao ni wa kwanza wa aina yake katika ulimwengu wa Kiarabu na Afrika.

Mashindano hayo matatu yanawakilishwa katika michuano ya kimataifa ya Misri kuanzia Februari 11 hadi 15, Mashindano ya Kimataifa ya Parataekwondo ya Misri Februari 16, na Kombe la Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Taekwondo kuanzia Februari 17 hadi 18, 2023.

Mashindano hayo ni ya juu zaidi kwani michuano ya kimataifa ya Misri imeainishwa G1 (pointi 10) na Kombe la Rais wa Shirikisho la Kimataifa limeainishwa G2 (pointi 20), na wachezaji watakaoshinda wanapata pointi 30, jambo linalosaidia wachezaji kuboresha uainishaji wao wa kimataifa na Olimpiki, na inatarajiwa kuwa kutakuwa na ushiriki mkubwa wa wachezaji kutoka nchi mbalimbali, na mashindano haya yanakuja sambamba na sherehe za Shirikisho la Kimataifa la Taekwondo la maadhimisho yake ya miaka hamsini kwa uanzishaji wake.

Kwa mara ya kwanza, kitengo cha Mashindano ya Kimataifa ya Parataekwondo ya Misri G1 (alama 10) kinatanguliwa na kamati ya uainishaji wa wachezaji, ambayo haikufanyika wakati wa mashindano yoyote ya kimataifa yaliyofanyika Aprili mwaka jana.

Hiyo inakuja ndani ya mfumo wa sera ya Wizara ya Vijana na Michezo inayolenga kuandaa michuano mbalimbali ya Kiarabu, bara, kikanda na kimataifa katika ardhi ya Misri kwa kuzingatia maagizo ya uongozi wa kisiasa, na kutokana na mambo ambayo Misri inafurahia kutokana na miundombinu ya michezo iliyojengwa kwa mujibu wa vipimo na viwango vya kimataifa.

Back to top button