Utambulisho Wa Kimisri

Maspero

Historia ya zamani sana na Hazina kubwa ya kazi inayoendelea tangu miaka 62.

 Kabla ya miaka 62 , ilipokuwa matangazo ya kwanza ya televisheni ya kimisri , kusherehekea kumbukumbu ya nane kwa maandamano ya 23 Julai , saa moja jioni, Julai 21 , 1960 Runinga ya kimisri ambayo hubeba jina la ” televisheni ya kiarabu ” ilizindua aya za Quran tukufu ,kisha kuonekana kwa Rais marehemu Gamal Abd El Nasser wakati wa ufunguzi wa baraza la umma na hotuba aliyeitoa mnamo siku hiyo na wimbo wa kitaifa ( Nchi yangu kubwa ) .

Matangazo yalifunguliwa kwa mara yake ya kwanza kwa muda wa masaa matano tu , yalihitimishwa kwa kusoma kwa Quran tukufu baadaye ya redio ya habari , mwanzoni televisheni ilikuwa kujumuisha kipindi kimoja , kilichokuwa kuendelea masaa sita kila siku , kisha masaa yaliongezeka hadi masaa kumi na tatu kila siku baada ya kuanzisha kipindi kingine cha runinga mnamo tarehe 21 Julai, 1961 , na imetumiwa kipindi cha tatu mnamo Oktoba 1962 na wastani ya masaa ya matangazo kwenye vipindi  vitatu ilikuwa kati ya masaa 25_30 kila siku .

Mwanzo wa kufikiria

Uanzishaji mnamo mwaka wa 1960 haukuwa kwa ghafla , basi uamuzi huo ulichukuliwa katikati ya miaka ya  hamsini , ila hali za kisiasa na uchokozi wa nchi tatu mwaka 1956 zilisababisha kuchelewesha kazi ya kuanzisha hadi mwaka 1959 , wakati ambapo Misri ilisaini mkataba  pamoja na shirika la redio la Marekani”RCA” ili kuongeza mtandao wa runinga ndani ya nchi , uundaji wa jengo la redio na televisheni ulimaliza mnamo 1960 katika makao makuu yake ya kisasa katikati ya Kairo huko kornesh El Nile .

Mwaka 1951 ulikuwa jaribio la kwanza la televisheni nichni Misri , ambapo kampuni ya kiufaransa ya utengenezaji wa redio na televisheni ilifanya jaribio la kwanza la matangazo ya televisheni huko Kairo , ili kupiga picha za sherehe zilizofanyika kwa hafla ya harusi ya Mfalme Farouk , kampuni ilipanga sherehe ya ndani ilihudhuriwa na wanachama ambao wana bahati ya kuweka vyombo vya upokeaji katika klabu zao .

 Mnamo 1954 , Salah Salem waziri wa mwongozo wa kitaifa wakati huo , alimwambia Rais Gamal Abd El Nasser jambo la kuanzisha jengo jipya la redio na kituo cha runinga juu ya mlima wa Mokatam na kilifanyika kwa kweli , na mnamo 1959 uanzishaji wa jengo la runinga  ulianza katika mahali ambapo lilijengwa hivi sasa , ili kuzindua matangazo yake mwaka 1960  , studio za runinga zilikuwa kuandaliwa na majaribio ya kwanza katika jukwaa la jumba la Abdin . Mnamo Agosti  13, 1970 amri mpya ya shirikisho la redio na televisheni ya kimisri (ERTU) iliundwa , na sekta nne zikiundwa : sekta ya redio , sekta ya runinga , sekta ya uhandisi , sekta ya kufadhili , na kila sekta ina Rais , na baada ya vita vya 1973  matangazo ya runinga na vifaa vya utangazaji yamebadilishwa , na kuwa yenye rangi chini ya mpangilio wa “SECAM ” , na matangazo ya kimisri ya runinga yamebadilishwa kutoka kwa mpangilio wa SECAM kuwa BAL mnamo 1992 .

Kuwepo vipindi kadhaa

Mnamo 1973 runinga ya kimisri ilianza opereseheni kubwa zaidi ili kuboresha vyombo vya matangazo , na mnamo 1978 vipindi viwili vya kwanza na vya pili viliunganishwa na eneo la Kanah , wakati ambapo kuanzisha kituo cha runinga kwa vipindi hivyo viwili katika Suez na Ismaalia na Port Saïd , Mnamo 1988 ilianza matangazo ya runinga kwa kipindi cha tatu kinachotolewa kwa kanda ya Kairo kubwa , mnamo mwaka huohuo kipindi cha nne kilizinduliwa kwa kanda ya Kanah “Mfereji wa Suez” .

Mnamo 1990 matangazo ya runinga  ya kipindi cha tano kinachowekwa kwa Aleskandaria yalianza , na mnamo 1994 ilizinduliwa ishara ya matangazo ya majaribio kwa kituo cha sita kwa katikati ya Delta na makao makuu yake huko Tanta , kinachotolewa kwa Gharbia , Dakahlia , Monifia , Kafr El Sheikh na Domyat , Mnamo 1994 matangazo ya kipindi cha saba kilianza na makao makuu yake  huko Minya na hushughulikia mikoa ya kaskazini ya Misri ya juu kama Bannysuif , Minya , Fayum na Asyout .

Mnamo 1996 ili kuwa kufunguliwa kituo cha nane na makao makuu yake ni Aswan na hutolewa kwa ajili ya mikoa ya kusini ya Misri kama Souhag , Qena , Aswan na Luxor .

Matangazo ya Sputniki

Wakati vituo vya Sputniki na sekta ya Nile kwa vituo maalum huanza matangazo yake mnamo 1990 ,  wakati ambapo kipindi cha kimisri cha kwanza kilikuwa kituo cha satellite cha kiarabu cha serikali cha kwanza kutolewa mnamo 1990 , kituo cha Nile cha kimataifa kilianza mnamo 1994 .

Kituo cha kimisri cha Sputniki cha pili kilianza kama kituo cha kwanza cha kiarabu kilichokuwa na msimbo na kuingia vyombo vya habari vinavyolipwa mnamo 1996 , kisha kuonekana kwa sekta ya Nile Kwa vituo maalum inayojumuisha vituo kadha vya michezo, habari , utamaduni , habari tofauti, mtoto na  vipindi vya mafunzo , baadaye hujumuisha sinema , vichekesho na burudani ( moja kwa moja ) , na cha mwisho kituo cha Maspero Zamani kilichokaribishwa sana kwa ubora wake katika uwasilishaji wa mada za kumbukumbu vya zamani kutoka vipindi , mifululizo na filamu zenye historia .

Shirika la vyombo vya habari la kitaifa

Maspero ina vipindi vinane vya kitaifa , na vingine kwenye Sputniki  , vingine vya redio , pia ina tovuti nyingi za vyombo vya habari na sekta za kiidara ni tovuti ya vituo vya runinga ya kimisri , runinga ya Nile , runinga ya Mahrosa , kituo cha habari za Misri , sekta ya redio, sekta ya uchumi , sekta ya usalama , na sekta ya uaminifu , na idadi ya wafanyikazi wake ni wafanyikazi elfu 34 ,pia inafuatiliwa na kampuni tano  nazo ni ” Nile sat ” , jengo la uzalishaji wa habari , kampuni na Shirika la Sot El Kahera , kampuni ya CNE na kampuni ya redio ya Nile iliyoboreshwa .

Mawaziri kumi na tisa walipata nafasi ya waziri wa wizara ya vyombo vya habari tangu kuanzisha shirikisho la redio na televisheni , waziri  wa kwanza alikuwa Mohemed Abd El Kader Hatem , lakini waziri wa mwisho ni Doria Sharf Eldin ,  wakati ambapo wizara ya vyombo vya habari na shirikisho la redio na televisheni zimefutwa kulingana na sheria ,namba 92 kwa mwaka wa 2016 kwa utaratibu wa taasisi kwa vyombo vya habari , na  badala ya hivyo shirika la vyombo vya habari la kitaifa lilikuja linaloongozwa sasa na Hessin Zien .

Vituo vya Idhaa kuu

Maspero inajumuisha karibu  na vituo 14 vikuu vya redio navyo ni : redio ya programu kuu 1934 , redio ya sauti ya Al Arab 1953 , redio ya mashariki ya kati 1964 ,  idhaa ya programu ya kiutamaduni _ programu ya pili hapo awali 1957 , redio ya vijana na michezo 1975 , redio ya muziki , redio ya programu ya Ulaya , redio ya Quran tukufu na redio ya nyimbo za kimisri _ ya maalum hapo awali 2000 .

 Vilevile inajumuisha redio ya habari na muziki 2000 , redio ya kielimu , redio zilizoelekezwa , redio za kikanda, redio ya Misri_inayofuata sekta ya habari sasa hivi , pamoja na vituo vinne vyenye ushirikiano kwa kiasi_vinavyofuata tovuti za redio ya Nile navyo ni Mega FM , redio HITS , NAGHAM FM na redio ya umma.

 

 

Chanzo: Tovuti ya Harakati ya Nasser kwa Vijana

Check Also
Close
Back to top button