Utambulisho Wa Kimisri

Benki ya Maarifa ya Kimisri

Wakati wa mfumo wa mpango wa mheshimiwa rais wa Jamhuri uliozinduliwa katika idi ya sayansi, mwaka wa 2014 kwenye jamii ya Kimisri hujifunza hujifikiri na hutengeneza, na pia kutoa misaada kwa juhudi za uboreshaji wa jamii ya maarifa ya Kimisri na kuongeza hamu ya raia wa Misri kwa sayansi na kutoa misaada kwa elimu na utafiti wa kisayansi, benki ya maarifa ya Kimisri imeandaliwa, mwezi wa Januari 2016, kama moja ya miradi muhimu ya kitaifa ya maarifa na kubwa zaidi katika sekta ya elimu na utafiti wa kisayansi katika historia ya kisasa ya Kimisri.

Benki ya maarifa ya Kimisri ina tovuti mbili kuu, kila tovuti inagawanya kwenye idadi ya tovuti ndogo.

Tovuti kuu ya kwanza ni tovuti ya upatikanaji wa habari ( www.ekb.eg) na inazingatia mojawapo mikataba ya namba kubwa zaidi na kituo cha maarifa cha kielektroniki kwenye ngazi ya kimataifa ambayo hutoa upatikanaji bure kwa machapisho ya elimu na kisayansi katika sekta nyingi za maarifa kwa wananchi wote ndani ya Jamhuri ya Misri ya kiarabu kwa usajili kwa kutumia nambari ya kitaifa , barua pepe na baadhi ya takwimu za kibinafsi na za kazi, tovuti hiyo inatoa huduma zake kupitia tovuti nne ndogo kwa wasomaji, watafiti, wanafunzi , walimu na pia watoto.

Huku tovuti kuu ya pili ya benki ya maarifa ya Kimisri ni tovuti ya uzalishaji na usambazaji wa habari za kitaifa za kitaaluma kwa vyuo vikuu vya Kimisri, vyuo, vituo vya utafiti na shirika lolote la utafiti au chuo ndani ya Jamhuri ya Misri ya kiarabu kupitia mfumo wa kuchapisha kielektroniki kulingana na viwango vya kimataifai, na tovuti hiyo inajumuisha mfumo ili kuunga mkono mtaala wa maarifa ya kisayansi na utafiti kwa vyuo vikuu vyote na vyuo vya utafiti unaosaidia kumbukumbu ya Kimisri ya kisayansi na utafiti kupitia ifuatavyo :

1- mfumo wa uongozi wa majarida ya kisayansi, kuashiria kwake na kuhifadhi kwake kwa elektroniki.

2- mfumo kwa uongozi wa mikutano inayojumuisha udhibiti wa mashindano ya kisayansi, maeneo ya kazi ya mikutano na usajili wa washiriki na uongozi wa maonyesho, na pia uongozi wa mfumo wa  kuchapisha.

3- mfumo wa tathmini ya matokeo ya kisayansi ya kitaifa kwa utafiti kupitia mfumo wa kipekee unaundwa kwa mashirika ya kisayansi ili kusimamia na kutathmini majarida ya kisayansi na kitaifa.

4- mfumo wa kuhifadhi na kusanya matokeo ya kitaifa kama aina ya kitaifa kwa watafiti wote kwenye ngazi ya Jamhuri.

5- kuhifadhi na kurejea kwa takwimu zote kupitia mfumo kuu pamoja na udhibiti wa uongozi wa mfumo huo.

Benki ya maarifa ya Kimisri kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya juu na elimu ya kiufundi inaonyesha vyanzo vingi vya habari za maarifa, elimu na utafiti vinavyoandikwa kwa maeneo makubwa ya kuchapisha kwenye ngazi ya kimataifa kulingana na makundi ya umri na elimu kwa lugha mbili za Kiarabu na Kiingereza kuanzia hadithi za watoto zinazosawiriwa na zenye sauti, na pia maarifa ya kisayansi mbalimbali na vyanzo vya kumbukumbu na hata majarida ya kisayansi, vitabu na barua za chuo kikuu, pia benki ya maarifa ya Kimisri inafanya warsha za kikazi na huduma za kuchapisha za kisayansi kwa ushirikiano kwa  maeneo ya utaalamu na kuchapisha – hiyo kama mfano – kwa taasisi mbalimbali za vyuo vikuu na wizara za nchi na taasisi za jeshi la Kimisri.

Katika mabadiliko ya mfumo wa elimu ya kisasa, benki ya maarifa ya Kimisri kwa ushirikiano na shirika la (CDSM) inaunga mkono mpango wa mabadiliko ya elimu ambayo ni kabla ya elimu ya juu, mpango unaolenga uboreshaji wa utumiaji Teknolojia katika elimu.

Katika uungaji mkono wa mpango wa utafiti wa Jamhuri ya Misri ya kiarabu na uainishaji wa vyuo vikuu vya Misri, benki ya maarifa ya Kimisri kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kisayansi na vyuo vikuu vya Kimisri inaunga mkono uzinduzi wa mfumo muhimu ili kupima utendaji wa utafiti wa vyuo kupitia takwimu (scival) inayopatikana na shirika la (elesiver) inayoongoza wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kisayansi na vyuo vikuu vya Kimisri.

Benki ya maarifa ya Kimisri hivi karibuni kwa ushiriki wa shirika la (clarivate analytics) na shirika la (jumba la mfumo) zimefanya kielelezo cha kwanza kwa lugha ya kiarabu (Arabic citation index) na itazinduliwa mnamo mwaka wa 2020 kama sehemu ya mitazamo ya Misri 2030 ili kugeuza Misri kwa uchumi unategemea maarifa, na hii itakuwa Njia ya kwanza ya kuorodhesha matokeo ya utafiti wa kisayansi kwa lugha ya kiarabu kwenye kielelezo cha nukuu za kumbukumbu, na itakuwa kupatikana kwa kutumia na utafiti kwa lugha mbili za Kiarabu na Kiingereza kwa taasisi zote za utafiti na chuo kwenye ngazi ya kimataifa kupitia takwimu ya tovuti ya kisayansi (web of science) na hii ni mmoja wa wachapishaji zaidi ulimwenguni na wa pekee katika sekta ya kielelezo cha nukuu za kumbukumbu za upande wowote, na itaunga mkono kielelezo cha nukuu za kumbukumbu kwa lugha ya kiarabu ili kutumiwa na watafiti wa Kimisri na hata katika nchi 22 ambazo ni wanachama wa chuo kikuu cha mataifa ya kiarabu.

Check Also
Close
Back to top button