Waziri wa Mambo ya Nje aelekea mji mkuu wa Tanzania kushiriki katika sherehe ya Bwawa la Julius Nyerere
Ahmed Hassan

Waziri wa Mambo ya Nje, Sameh Shoukry anaongoza ujumbe rasmi wa Misri unaoelekea mji mkuu wa Tanzania Dar El-Salam ; kuhudhuria sherehe ya kujaza maji katika ziwa la Bwawa la Julius Nyerere linalotekelzwa na Muungano wa Misri wa makampuni mawili nayo ni: Al-muqwilan Al-arab na Elsewedy Electric kwenye mto wa Rufijii nchini Tanzania .
Pia Mheshimiwa Balozi Abu zed, Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje alieleza kuwa imepengwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anashiriki katika sherehe hiyo kwa sababu mradi huo una umuhimu mkubwa kwa Watu wa Tanzania .
Inaashiriwa kuwa Bwawa hilo linazingatiwa moja ya miradi muhimu zaidi ya kimaendeleo Barani Afrika na mfano wa kuigwa wa Ushirikiano wa kikanda kati ya nchi zote za Afrika ndugu ili kuendeleza juhudi za maendeleo na kufikia maslahi ya watu wake .