Habari

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akutana na Madaktari Bingwa Mjini Alexandria

0:00

 

Mhe. Balozi Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri akiwa na Maafisa wa Ubalozi ameonana na Madaktari bingwa kutoka Tanzania wanaosoma Chuo Kikuu cha Alexandria huko Tolip Hotel, Mjini Alexandria siku ya tarehe 12 Januari, 2024 kwa lengo la kujitambulisha kwao na kufahamiana.

Aidha, wanafunzi hao walitumia fursa hiyo kumweleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na ongezeko la ada ya usajili ya USD 1,820 inayolipwa Wizara ya Elimu ya Misri ambayo haikuwepo kabla.

Changamoto nyengine ni kutofahamishwa hadi leo majina ya Wanafunzi waliopata ufadhili kupitia Samia Superspecialists Acholarship iliyoanzishwa na Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hali ambayo inawapa shida kuendelea na masomo yao.

Hivyo, walimuomba Balozi kuwasaidia kutatua changamoto hizo. Nae, Mhe. Balozi aliahidi kufuatilia changamoto hizo na kuwakumbusha dhima kubwa waliyonayo kwa Jamii ikizingatiwa Tanzania inasherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyolenga kumuondoa Mtanzania katika utawala wa kisultan ili apate huduma bora za kijamii, elimu pamoja na afya.

Aliwaasa Madaktari hao kujitahidi kuzingatia masomo, kufahamu wanachosomeshwa ili wakirudi nyumbani watoe huduma bora kwa jamii kwa sababu Serikali zetu zote mbili zinatumia fedha nyingi kuwasomesha Madaktari hao.

Back to top button