Balozi wa Tanzania atembelea Mamlaka za Mamlaka za Bandari nchini Misri

Siku ya tarehe 14 Januari, 2024 Mhe. Mej. Gen. Richard M. Makanzo aliweza kuonana na Rear Admiral Reda Ahmed Ismail, Kiongozi Mkuu wa Sekta ya Usafirishaji Baharini nchini Misri kwa lengo la kuimarisha Uhusiano na Ushirikiano baina ya Mamlaka za Usafirishaji Baharini nchini Misri na Mamlaka za Tanzania ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam Maritime Institute, SUMATRA, TASAC, Tanzania Port Authority na Zanzibar Maritime Authority.
Naye, Bw. Reda Ismail alieleza kufurahishwa na ziara hiyo na kusema Uwepo wa mashirikiano mazuri baina ya taasisi za Tanzania na Misri kutaongeza chachu ya uhusiano na ushirikiano, biashara na kufungua masoko mapya kufuatia uwepo wa huduma za usafiri wa uhakika wa anga na Meli baina ya Misri na Tanzania.
Bw. Reda alieleza uwepo wa ‘draft’ MoU baina ya Wizara za Uchukuzi za Nchi mbili hizi iliyogusa maeneo mbali mbali muhimu ya ushirikiano.
Hivyo, alishauri uwepo wa haja ya pande mbili kukamilisha utiaji saini MoU hiyo na kuanza utekelezaji wake mara moja.
Pia, alishauri kufanyika kikao haraka kupitia mtandao (online meeting) kitakachohusisha Wizara na Mamlaka mbali mbali za usafirishaji baharini.