Balozi wa Tanzania aonana na Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Alexandria

siku ya tarehe 14/01/22024 Mhe. Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo alikamilisha ziara yake Mjini Alexandria kwa kuonana na Prof. Hisham Said, Makamo Mkuu wa Chuo cha Alexandria University ambacho Madaktari Bingwa kutoka Tanzania wanapata Taaluma hapo.
Mhe. Balozi Richard Makanzo alimpongeza Prof. Hisham na Uongozi mzima wa Alexandria University kwa kazi kubwa wanayoifanya kuwapatia taaluma wataalam hao muhimu katika Jamii kupitia Makubaliano yaliopo katika sekta ya elimu baina ya Misri na Tanzania.
Sambamba na hilo, Mhe. Mej. Gen. Richard Makanzo aliuomba uongozi wa Chuo kuwasaidia Wanafunzi wa Tanzania kuwaondoshea mzigo wa malipo ya USD 1820 ambazo hazikuwepo kabla na hazimo katika barua za udhamini wao, malipo ambayo yamewekwa na Wizara ya Elimu mwaka huu kwa mara ya kwanza bila ya kupewa taarifa.
Nae Prof. Hisham alieleza ni kweli yapo maelekezo ya Wizara ya Elimu kuwataka Wanafunzi kulipa USD 1820, hata hivyo Chuo imeliona tatizo hilo na mazungumzo yanaendelea baina cha Baraza la Chuo na Wizara ya Elimu kuomba malipo hayo yaondolewe kwa kuwa wanafunzi hao wanasoma kupitia mpango maalum wa udhamini na hayamo katika makubaliano.
Pia, alieleza Chuo kinaendelea kuwasomesha wanafunzi walioathirika na utaratibu hio mpya bila ya matatizo yoyote na baada ya kukamilika mazungumzo yanayoendelea, ada hiyo mpya itafutwa kupitia agizo maalum kutoka kwa Waziri Mkuu wa Misri, Mhe Moustafa Madbouli.
Ziara ya Mhe. Balozi Mej. Gen. Richard Makanzo Mjini Alexandria imekuwa na mafanikio makubwa kwa kufungua maeneo mapya ya ushirikiano miongoni mwa Taasisi mbali mbali za Elimu ikiwa ni pamoja na chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha SUZA Zanzibar, Chuo Kikuu cha Dodoma na Mamlaka za Usafirishaji kwa kutukia Bahari. Ziara hiyo imefanyoka tarehe 12 hadi 14 Januari, 2024.
Mhe. Balozi aonana na Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Alexandria